Nenda kwa yaliyomo

Mau Mau

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Maumau)
Vikosi vya KAR

Mau Mau lilikuwa kundi la wapiganaji wa Kenya waliokuwa wakipinga utawala wa kikoloni wa Waingereza toka mwaka 1952 hadi 1960. Harakati zao (kwa Kiingereza: Maumau uprising, Maumau rebellion) ziliongozwa na Wakikuyu na zilitokana na wingi wa watu kutoridhika kuhusu kupokonywa ardhi, ukandamizaji wa kisiasa, na kukosa usawa wa kijamii. Vikatokea vita vya kishujaa na matendo ya uharibifu dhidi ya serikali ya kikoloni na wakoloni wenyewe.

Waingereza walijibu kwa mbinu kali za kijeshi, zikiwa ni pamoja na kazi ya lazima, mateso ya watu wengi, na mauaji[1].

Urithi wa uasi huu bado ni kipengele muhimu katika historia ya Kenya, ikiashiria upinzani dhidi ya ukoloni na mapambano ya kudai haki. Ingawa vuguvugu la Mau mau halikuwa na mafanikio makubwa kijeshi, upinzani wao ulichangia sana katika kuharakisha upatikanaji wa uhuru wa Kenya mwaka 1963.

Chanzo cha jina la kundi hili, Mau mau, hakieleweki vyema. Kuna hali ya kutokukubaliana juu ya chanzo na maana ya jina lenyewe. Baadhi wanadai kuwa ni jina la vilima fulani huko Kenya, wengine wanaamini kuwa jina hilo lilitoka kwa walowezi wa Kiingereza lililokuwa na nia ya kudhalilisha kundi hilo. Wako pia wanaosema kuwa jina hilo ni kifupi cha: "Mzungu Aende Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru".

Sehemu kubwa ya kundi la Mau mau iliundwa na watu wa kabila la Gikuyu huku kukiwa na baadhi ya wanachama toka Embu na Meru. Wakikuyu wenyewe hawakuwa wakiliita kundi hili Mau mau bali "Muingi" (vuguvugu), "Muigwithania" (anayeunganisha), "Muma wa Uiguano" (kiapo cha umoja) au KCA (Kenya Central Association, chama kilichotangulia kupigania haki za Wakikuyu.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kundi lilianzishwa mwaka wa 1946, na viongozi wake walikuwa Jomo Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga, Paul Ngei, Ronald Ngala, Harry Thuku na wengineo. Walionyesha watu wanavyoweza kufika mbali wakiwa kitu kimoja.

Hata hivyo, katika kuhamasisha wananchi wenzao walitumia shuruti na kuua maelfu [2] ya waliokataa kuwaunga mkono [3], hasa walipodaiwa kula kiapo cha kukana imani ya Kikristo na cha kuwa tayari kuua [4]. Mmojawao ni Aloisio Kamau [5].

  1. ↑ "Mauaji makubwa ya Uingereza".
  2. ↑ Anderson 2005, p. 84.
  3. ↑ "Histories of the Hanged: The Dirty War in Kenya and the End of Empire" (PDF). uk. 175. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka (PDF) kutoka chanzo mnamo 24 Juni 2023. Iliwekwa mnamo 24 Juni 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. ↑ John Baur, 2000 Years of Christianity in Africa - An African Church History, 2nd ed., Nairobi 2009, p. 342
  5. ↑ Aloisio Kamau shahidi wa imani - Consolata Missionary Sisters, Nairobi

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: