Nenda kwa yaliyomo

Luteni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama kwenye sare ya luteni katika jeshi la Tanzania.

Luteni (kutoka Kiingereza: Lieutenant), pia Luteni wa Kwanza, ni cheo cha afisa wa jeshi kilicho chini ya Kapteni na juu ya Luteni wa Pili.

Asili ya neno ni Kifaransa "lieu-tenant" (yaani "mwenye kushika nafasi") kwa maana ya naibu, makamu. Kiasili lieu-tenant alikuwa makamu wa kapteni, yaani mkuu wa kikosi aliyeshika mamlaka yake wakati hayuko.

Maana hiyo ni pia asili ya vyeo vya Luteni Kanali au Luteni Jenerali vilivyotaja manaibu wa kanali au jenerali.

Baadaye ziliendelea kuwa vyeo vya pekee bila kuunganishwa na nafasi ya makamu tena.

Majeshi ya Afrika yalirithi cheo hicho sawa na vyeo vya kijeshi kwa jumla kutoka mapokeo ya jeshi la kikoloni.

Vyeo vya kijeshi - Tanzania

Jenerali * Luteni Jenerali * Meja Jenerali * Brigedia * Kanali * Luteni Kanali * Meja * Kapteni * Luteni * Luteni-usu

Afisa Mteule Daraja la Kwanza * Afisa Mteule Daraja la Pili * Sajinitaji * Sajenti * Koplo * Koplo-usu