Reli ya SGR Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Reli ya SGR Tanzania au Reli ya geji sanifu ya Tanzania ni mradi wa kuunganisha Tanzania na nchi jirani kwa njia ya reli ya geji sanifu. Njia ya geji sanifu inalenga kufika Rwanda na Uganda, na kupitia nchi hizi mbili, hadi Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Reli mpya ya geji sanifu imekusudiwa kuchukua nafasi ya mfumo wa reli ya zamani inayotumia geji ya mita moja.[1] [2] Inaendeshwa na Shirika la Reli Tanzania (TRL).

Mahali[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa reli umepangwa kuwa na sehemu kuu zifuatazo:

Sehemu ya Dar es Salaam-Morogoro[hariri | hariri chanzo]

Sehemu hii yenye urefu wa km 300, ilianza kujengwa na ushirikiano wa makampuni ya Yapi Merkezi kutoka Uturuki na Mota-Engil ya Ureno. Ujenzi ulianza mwezi Aprili 2017. [2] Ujenzi umefadhiiwa kwa njia ya mkopo wa dolar za Marekani bilioni 1.2 kutoka Eximbank ya Uturuki. [3] Kufikia Februari 2019, asilimia 42 ya kazi kwenye sehemu hii iliripotiwa kuwa kamili. [4] Mnamo Mei 2019, ilitangazwa kuwa asilimia 60 zilikamilika na kwamba treni za kwanza za abiria zilitarajiwa kuanza huduma mnamo Desemba 2019. Kwenye mwezi wa Oktoba serikali ilitangaza mchakato wa kununua mabehewa ya mizigo 1,430, injinitreni 20 na mabehewa ya abiria 60[5].

Katika Novemba 2019 TRC ilieleza kuwa kazi zimecheleweshwa na mvua ilhali asilimia 70 zilikamilika.

Mpango wa awamu la kwanza una vituo sita: Dar es Salaam, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro . Treni tatu zimepangwa kusafari pande zote kila siku. [6]

Sehemu ya Morogoro-Dodoma-Makutopora[hariri | hariri chanzo]

Ushirikiano wa Yapi Merkezi na Mota-Engil ilipewa pia kazi kwa awamu ya pili kutoka Morogoro kupitia Dodoma hadi Makutopora (Manyoni, Singida) kwa urefu wa km 426. [7] Ujenzi huu uangharamiwa kupitia mkopo kutoka Benki ya Standard Chartered wa dolar bilioni 1.46. [3]

Mpango wa awamu la pili una vituo vifuatavyo: Morogoro, Mkata, Kilosa, Kidete, Gulwe, Igunda, Dodoma, Bahi na Makutopora,

Sehemu ya Makutopora-Isaka[hariri | hariri chanzo]

Sehemu hii, yenye urefu wa km 435 kutoka Makutopora kupitia Tabora hadi Isaka bado haijapewa mkandarasi wakati wa Septemba 2018. [3]

Sehemu ya Isaka-Mwanza[hariri | hariri chanzo]

Vilevile sehemu ya km 220 kutoka Isaka hadi jiji la Mwanza, kwenye mwambao wa kusini mwa Ziwa Viktoria [8] haiuwa na makndarasi bado wakati wa Septemba 2018. [3]

Sehemu ya Isaka-Rusumo[hariri | hariri chanzo]

Mkono mwingine unapangwa kuendelea kutoka Isaka hadi Rusumo kwenye mpaka wa Rwanda, kwa jumla kuelekea Kigali. Sehemu hii ina urefu wa km 371. Ujenzi wa sehemu hii umekadiriwa kufika dolar milioni 942 za Marekani. [9] Mnamo Aprili, gazeti la EastAfrican liliripoti kwamba Benki ya Dunia imeelezea nia yao ya kufadhili reli ya Isaka-Kigali Standard Gauge. [1]

Maelezo ya jumla[hariri | hariri chanzo]

Hii njia ya reli yenye geji sanifu ya milimita 1,435 inalenga kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa kati ya bandari ya Dar es Salaam na Kigali, nchini Rwanda, baadaye pia na Bujumbura, nchini Burundi, na hatimaye Goma katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo . Kutoka bandari ya ziwa ya Mwanza, feri za Ziwa Viktoria zinatarajiwa kusafirisha bidhaa kati ya Mwanza na Port Bell karibu na jiji la Kampala, mji mkuu wa Uganda. [10] [11] [12]

Treni za mfumo wa SGR nchini Tanzania zitatumia umeme. [13]

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. 1.0 1.1 Olingo (29 April 2018). Tanzania turns to World Bank to fund its modern railway project. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 2. 2.0 2.1 TanzaniaInvest.com (14 April 2017). Dar Es Salaam-Morogoro Standard Gauge Railway Works Start. TanzaniaInvest.com. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 3. 3.0 3.1 3.2 3.3 Olingo (15 September 2018). Tanzania secures $1.46 billiob SGR loan from Stanchart. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 4. Nachilongo (12 February 2019). Construction of Dar-Moro SGR reaches 42pc. Iliwekwa mnamo 16 February 2019.
 5. Tanzania Standard Gauge Railway to Start Operations in December 2019 (en-US). TanzaniaInvest (2019-07-10). Iliwekwa mnamo 2019-11-03.
 6. Allan Olingo (11 May 2019). Dar SGR project inches closer to reality as locomotives to test phase one arrive. Iliwekwa mnamo 12 May 2019.
 7. Xinhua (15 March 2018). Tanzanian president launches construction of new phase of standard gauge railway. Xinhua. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 8. Globefeed.com (16 September 2018). Distance between Isaka, Tanzania and Mwanza, Tanzania. Globefeed.com. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 9. Kabona (29 January 2018). Isaka-Kigali SGR works to start in October. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 10. Barigaba (27 June 2018). Uganda resumes cargo operations on Lake Victoria after a decade. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 11. Tairo (9 July 2018). Tanzania unveils cargo train to Uganda. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 12. The Citizen Reporter (27 June 2018). Tanzania's MV Umoja resumes Port Bell-Dar route after 10 years. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.
 13. Olingo (18 March 2018). Rwanda, Tanzania agree on electric SGR, opt for open tender. Iliwekwa mnamo 16 September 2018.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]