Nenda kwa yaliyomo

Bujumbura

Majiranukta: 3°23′S 29°22′E / 3.383°S 29.367°E / -3.383; 29.367
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bujumbura, Uganda

3°23′S 29°22′E / 3.383°S 29.367°E / -3.383; 29.367


Jiji la Bujumbura
Jiji la Bujumbura is located in Burundi
Jiji la Bujumbura
Jiji la Bujumbura

Mahali pa mji wa Bujumbura katika Burundi

Majiranukta: 3°21′49″S 29°22′3″E / 3.36361°S 29.36750°E / -3.36361; 29.36750
Nchi Burundi
Mkoa Bujumbura Mairie
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 300 000
Tovuti:  www.villedebujumbura.org

Bujumbura, ni mji mkuu wa Burundi unaokadiriwa kuwa na idadi ya wakazi 300,000. Mji upo kaskazini mashariki mwa Ziwa Tanganyika, na ni mji mkubwa zaidi Burundi, kitovu cha mawasiliano na uchumi nchini humo.

Bujumbura ni mji pekee Burundi ambao una bandari ya kupakia mali na bidhaa mbalimbali za kuuza nje, kama vile kahawa, pamba, ngozi na madini ya stani.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Bujumbura ilipanuka toka ilipokuwa kijiji kidogo kilichokuwa kambi ya Jeshi ya Wajerumani. Eneo hili lilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani mwaka wa 1889.

Lakini, baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Bujumbura ilichukuliwa na Ubeljiji ambapo Shirikisho la Mataifa ilisimamia Ruanda-Urundi. Jina la mji likabadilishwa kutoka Usumbura hadi Bujumbura. Burundi ilipopata uhuru, mwaka wa 1962.

Bujumbura ni mji ambao umeshuhudia vita vya ukabila kati ya Wahutu na Watutsi kwa kung'ang'ania uongozi wa Burundi.

Vivutio[hariri | hariri chanzo]

Katika mji huo kuna majengo ni yale ya kikoloni na pia kuna soko, uwanja wa taifa, msikiti mkubwa na Kanisa kuu. Pia kuna Jumba la Makumbusho ambalo linaitwa jumba la makumbusho ya maisha na jumba la makumbusho ya jiologia.

Mambo mengine ya kuchangamsha ni kama Hifadhi ya Rusizi, na Kiamba hapo Mugere, ambapo panasemekana kwamba David Livingstone na Henry Stanley walikutana. (Lakini watu wengi wasema walikutana Ujiji), Kigoma, nchini Tanzania ambapo panasemekana ni mwanzo wa mto unaosemekana kuwa ndio mwanzo wa Mto Nile).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bujumbura kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.