Nenda kwa yaliyomo

Ruanda-Urundi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa Ruanda-Urundi kando la Kongo ya Kibelgiji
Ramani ya Ruanda-Urundi wakati wa ukoloni
Wafanyakazi wahamiaji wa kiruanda katika mgodi wa Kisanga huko Katanga(Kongo ya Ubelgij)

Ruanda-Urundi ni jina la zamani kwa ajili ya nchi za Rwanda na Burundi. Zote mbili zilikuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi 1916. Wakatu wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia jeshi la Force Publique la Ubelgiji kutoka Kongo lilivamia maeneo yake; katika ugawaji wa koloni ya Kijerumani maeneo yale yalikubaliwa na Uingereza kubaki upande wa Ubelgiji.

Baadaye zilikabidhiwa na Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa kwa Ubelgiji. Ubelgiji ilitawala nchi zote mbili kama eneo moja la "Ruanda - Urundi". Hali halisi ziliangaliwa kwa muda mrefu kama eneo la nyongeza la Kongo ya Kibelgiji. Lakini hali yake katika sheria ya kimataifa kuwa eneo la kudhaminiwa iliizuia kuunganishwa rasmi na koloni ile kubwa.

Nchi zote mbili zilitawaliwa kwa mfumo wa "utawala usio moja kwa moja" ihali Wabelgiji walitumia watawala wa jadi. Wafalme hao waliotwa Mwami walitoka kimapokeo katika kundi la Watutsi ilhali idadi kubwa ya wananchi walihesabiwa katika kundi la Wahutu. Makundi haya hayakuwa makabila tofauti maana walikuwa na lugha na utamaduni wa pamoja; walikuwa zaidi matabaka katika jamii ambayo yaliwahi kuanza karne kadhaa zilizopita kama makabila tofauti lakini zimeshaunganika kiutamaduni; hata hivyo yalikuwa tofauti kiuchumi kwa mkazo wa ufugaji upande wa Watutsi na ukulima upande wa Watutsi. Hata hivyo iliwezekana kwa Mhutu kupata ng'ombe wengi na kuitwa Mtutsi, na Mtutsi maskini kuanza kulima akitazamiwa kuwa Mhutu. Kisiasa tofauti ilisababishwa na mfumo wa utawala wa mwami (mfalme) aliyepaswa kuteuliwa kutoka familia za Watutsi.

Katika kipindi cha ukoloni uhusiano baina ya Watutsi na Wahutu ulibadilika kwa sababu wakoloni walitazama Watusi kuwa watu wa mbari wa juu. Waliimarisha tofauti kwa kuanzisha mfumo wa kuorodhesha na kutoa vitambulisho kwa wananchi ambako kila mtu aliandikishwa ama kama Mtutsi au Mhutu, na hivyo njia ya kuhama kundi ilifungwa. Wakipendelea Watutsi idadi ya Wahutu walioteuliwa kuwa mchifu wa maeneo ilipungua, hasa upande wa Rwanda.

Katika miaka ya 1950 elimu ya kisasa ilifanya Wahutu kudai haki za kisiasa sawa na Wahutu. Mwaka 1959 upinzani wa Wahutu dhidi ya utawala wa Watutsi uliendelea kwenye mapinduzi katika Rwanda ambako Mwami alipinduliwa na mauaji ya wapinzani wa kisiasa yalifanya Watutsi zaidi ya 100,000 kukimbia katika nchi jirani. Wakati huohuo uhusiano baina ya makundi ndani ya Burundi haukuonyesha mafarakano makali vile bado na mfalme wa Burundi alilenga kutengwa kwa Burundi na Rwanda.

Wakati wa mwisho wa utawala wa kikoloni kwenye mwaka 1961 sehemu zote mbili ziliachana na kuingia katika uhuru kama nchi mbili za Rwanda na Burundi. Burundi huru ilianza kama ufalme, ilhali Rwanda imeshakuwa jamhuri.

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]
  • Samson, Anne (2016).Samson, Anne (2016). "Ruanda and Urundi". 1914-1918 Online: International Encyclopedia of the First World War. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2019.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Chrétien, Jean-Pierre (2003). The Great Lakes of Africa: Two Thousand Years of History (toleo la English trans.). New York: Zone Books. ISBN 9781890951344.
  • Gahama, Joseph (1983). Le Burundi sous administration Belge: la période du mandat, 1919-1939 (toleo la 2nd rev.). Paris: Karthala. ISBN 9782865370894.
  • Louis, William Roger (1963). Ruanda-Urundi 1884-1919. Oxford: Clarendon Press.
  • Newbury, Catharine (1994). The Cohesion of Oppression: Clientship and Ethnicity in Rwanda, 1860-1960. New York: Columbia University Press. ISBN 9780231062572.
  • Pedersen, Susan (2015). The Guardians: The League of Nations and the Crisis of Empire. Oxford: Oxford University Press. ISBN 978-0-19-957048-5. {{cite book}}: Invalid |ref=harv (help)
  • Rumiya, Jean (1992). Le Rwanda sous le régime du mandat belge, 1916-1931. Paris: Éd. L'Harmattan. ISBN 9782738405401.
  • Vijgen, Ingeborg (2005). Tussen mandaat en kolonie: Rwanda, Burundi en het Belgische bestuur in opdracht van de Volkenbond (1916-1932). Leuven: Acco. ISBN 9789033456213.
  • Botte, Roger (1985). "Rwanda and Burundi, 1889-1930: Chronology of a Slow Assassination". The International Journal of African Historical Studies. 18 (2): 289–314. doi:10.2307/217744. JSTOR 217744.
  • Des Forges, Alison (2014). Defeat is the Only Bad News: Rwanda under Musinga, 1896-1931. Madison: University of Wisconsin Press. ISBN 9780299281434.