Injinitreni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
"Gari la mooshi - injinitreni ya mvuke

Injinitreni (pia: kichwa cha garimoshi; Ing. locomotive) ni sehemu ya treni yenye injini na nguvu ya kuvuta au kusukuma treni yote. Ni kama gari kubwa lisilobeba abiria au mizigo. Badala yake inabeba ndani yake injini moja au zaidi kubwa pamoja na tenki

Aina za injinitreni[hariri | hariri chanzo]

Injinitreni diseli[hariri | hariri chanzo]

Katika mazingira ya milima injiniterni 3 zimeunganishwa pamoja kuvuta treni ndefu haraka

Injinitreni ya diseli huwa na injini ya diseli. Kuna aina mbili

  • mara nyingi injini inasukumu magurudumu kupitia giaboksi.
  • aina nyingine inatumia nguvu ya injini ya diseli kwa njia ya jenereta kutumia umeme unasoendesha injini ya umeme.

Injinitreni ya mvuke[hariri | hariri chanzo]

Injinitreni ya mvuke

Injinitreni ya mvuke hutumia joto la kuwasha kuni, makaa au mafuta kuchemsha maji na kusukuma injini kwa nguvu ya mvuke wa maji.

Hii ilikuwa aina asilia ya injiniterni lakini siku hizi hazitumiwi tena isipokuwa mahali pachache kwa ajili ya maonyesho au utalii.

Injinitreni ya umeme[hariri | hariri chanzo]

Injinitreni umeme ya A GG1

Katika nchi nyingi injinitreni zinatembea kwa nguvu ya umeme inayopatikana kwa njia ya nyaya za umeme kando la njia ya reli.

Aina hii ina gharama ndogo kwa harakati lakini gharama ni kubwa kujenga nyavu ya umeme kando la njia za reli.