Mto Songwe (Songwe)
Mandhari
Kwa mto mwingine wenye jina hili, tazama Songwe (Mbeya).
Mto Songwe (au Songwe ya Kaskazini) ni kati ya mito ya mkoa wa Songwe (Tanzania Kusini Magharibi). Mto huo, ambao umeupa mkoa jina lake, una chanzo chake katika milima ya Umalila karibu na Santilya iliyopo kusini ya Mbeya ikielekea kaskazini na kuishia Ziwa Rukwa.
Bonde lake limejulikana kati ya wataalamu wa akiolojia kwa mifupa na mabaki ya nyakati za kale zinazopatikana hapa.
Barabara ya Mbeya kwenda Zambia inavuka mto Songwe penye kiwanda cha saruji inayotumia mawe ya bonde la mto.
Mto unapita baadaye karibu na kijiji cha Galula kabla ya kufikia ziwa Rukwa.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mto Songwe (Songwe) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |