Nenda kwa yaliyomo

Ruvuma (mto)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mto Ruvuma)
Mto wa Ruvuma
Chanzo Karibu na Songea kwa 10° 45' kus., 35° 40' mash.
Mdomo Bahari ya Hindi, kusini ya Mtwara kwa 10° 28' kus., 40° 30' mash.
Nchi Tanzania, Msumbiji
Urefu 1,083 km
Kimo cha chanzo 1,850 m
Mkondo ?? m³/s
Eneo la beseni 165,760 km²
Ramani ya Mto Ruvuma

Ruvuma (pia: Rovuma) ni mto mrefu wa Tanzania na Msumbiji. Mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji unafuata mwendo wake kwa km 730.

Chanzo chake kiko mashariki kwa mji wa Songea katika milima ya Matagoro upande wa mashariki wa Ziwa la Nyasa. Unaelekea magharibi kati ya vilima kwenye kimo cha mita 1000 karibu na Songea halafu unabadili mwelekeo kwenda kusini.

Unapofikia mpaka wa Tanzania na Msumbiji, takriban km 200 baada ya chanzo, unageuka tena kuelekea mashariki hadi bahari. Km 35 baada ya kuungana na mto Lujenda pana maporomoko ya Upinde.

Km 160 kabla ya kufika mdomoni bonde la Ruvuma linapanuka kuwa na upana wa km 10; lalio la mto ni karibu mita 500 likiwa na visiwa vya mchanga. Wakati wa ukame maji hupungua sana hadi watu kuvuka mto kwa miguu; wakati wa mvua umbali kati ya pande zote mbili unafikia zaidi ya kilomita moja.

Mdomo uko Bahari ya Hindi kati ya Mtwara (Tanzania) na Rasi ya Delgado (Msumbiji). Mdomo wenyewe una umbo la delta. Athira ya maji kujaa au kupwa baharini huonekana km 20 kabla ya mdomo wenyewe.

Kabla kufika kwenye delta kuna feri inayobeba magari kati ya Tanzania na Msumbiji. Feri ilipelekwa hapa na mapadre Wabenedikto wanaofanya kazi pande zote mbili za mto.

Matawimto muhimu ni mto Muhuwesi na mto Lumesule upande wa Tanzania, halafu mto Lucheringo na mto Lujenda upande wa Msumbiji.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

de: "Rowuma" - Deutsches Koloniallexikon (Kamusi ya koloni za Ujerumani 1914) [1] Ilihifadhiwa 23 Juni 2006 kwenye Wayback Machine.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ruvuma (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.