Tawimto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mstari buluu mnene ni mto mkuu, mstari mwembamba ni tawimto.

Tawimto[1] (ing. tributary) ni mto unaoishia katika mto mwingine na mkubwa zaidi.

Kwa kawaida maji ya eneo fulani hutiririka chini na kuwa vijito na mito hadi kuishia katika mto mkuu unaobeba maji yote hadi baharini, ziwa kubwa au wakati mwingine katika sehemu ya jangwa yanapopotea. Mto unaofikia mwishi hutazamiwa kuwa mto mikuu wa beseni, na yote mingini ni tawimito yake, ama moja kwa moja au kupitia tawimito mingine.

Wataalamu wakiorodhesha mito yote ya beseni ya mto fulani hutumia hasa taratibu miwili tofauti za kuorodhesha mito hii

  • hesabu kutoka chanzo cha mto mkuu kuelekea mdomono
  • hesabu kutoka mdomo wa mto mkuu

Tawimito huorodheshwa kuwa ya kushoto au kulia. Hapo msimamo daima hufuata mwelekeo wa maji kutoka chazo kwenda mdomoni. kwa mfano pala ambako mto Ruvuma ni mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji ukielekea Bahari Hindi, mito yote inayoingia Ruvuma kutoka upande wa Msumbiji ni tawimito ya kulia, tawimito yote inayoingia kutoka upande wa Tanzania ni tawimito ya kushoto.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Neno hili "tawimto" haikutumiwa sana bado na waandishi na wasemaji wa Kiswahili, ni kati ya istilahi za sayansi zilizopendekezwa na kamusi ya KAST.