Nyasa (ziwa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ziwa la Nyasa)
Rukia: urambazaji, tafuta
Mstari mwekundu unaonyesha mpaka usiokubaliwa kati ya Tanzania na Malawi. Tanzania inadai mstari mwekundu kuwa sahihi, lakini Malawi inadai ziwa lote hadi mwambao wa Tanzania. Mpaka kati ya Msumbiji na Malawi hauna matata.

Ziwa Nyasa (katika Malawi: Lake Malawi; katika Msumbiji: Niassa) ni kati ya maziwa makubwa ya Afrika ya Mashariki ikiwa na nafasi ya tatu baada ya Viktoria Nyanza na Ziwa Tanganyika.

Lina urefu wa 560 km na upana wa 50-80 km. Vilindi vyake vinaelekea hadi mita 704 chini ya uwiano wa maji yake.

Ziwa Nyasa linapatikana kati ya nchi za Malawi, Msumbiji na Tanzania.

Kusini mwa ziwa unatoka Mto Shire unaopeleka maji kwenye Mto Zambezi na hatimaye Bahari Hindi.

Kijiolojia ziwa ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.

Eneo la Ziwa[hariri | hariri chanzo]

Eneo la ziwa ni 29,600 km². Sehemu kubwa ni eneo la Malawi, robo ya kusini-mashariki ni eneo la Msumbiji, robo ya kaskazini-mashariki ni eneo la Tanzania. Lakini kuna ugomvi kati ya Malawi na Tanzania kuhusu mipaka. Malawi imedai ya kwamba maji yote hadi ufukoni upande wa Tanzania ni sehemu ya eneo lake la kitaifa. Tanzania imedai ya kwamba mpaka uwepo katikati kufuatana na uzoefu wa kimataifa.

Sababu ya mzozo ni utaratibu wa kikoloni. Wakati wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani palikuwa na mpaka wa kimataifa kaskazini mwa ziwa. Baada ya 1919 Uingereza ilitawala Tanganyika pamoja na Malawi (Nyasaland). Kwa kusudi la kurahisisha utawala mambo yote yaliyohusu ziwa yaliwekwa chini ya serikali ya kikoloni ya Nyasaland. Baada ya uhuru Malawi ilijaribu kutumia uzoefu huo kama haki yake ya kitaifa. Polisi yake ilijaribu kutawala wavuvi na feri za Tanzania ziwani. Mzozo huu ulisababisha risasi kufyatuliwa baada ya uhuru. Hadi leo hakuna mapatano rasmi lakini nchi zote mbili zinaendelea bila kutumia nguvu. Hali halisi Malawi imeheshimu dai la Tanzania halikusumbua tena wavuvu au feri za jirani ndani ya robo ya kaskazini-mashariki ya ziwa.

Ziwa Nyasa linajulikana kuwa na aina nyingi za samaki (zaidi ya 1500). Aina chache tu zinavuliwa kama chakula lakini aina mbalimbali zinakamatwa na kuuzwa nje ya Afrika kwa wapenzi wa samaki zenye rangi.

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyasa (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.