Nenda kwa yaliyomo

Galula

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Galula ni kata ya Wilaya ya Songwe katika Mkoa wa Songwe, Tanzania. Msimbo wa posta ni 53831.

Galula iko kwenye Mto Songwe, umbali wa takriban kilomita 18 kutoka Ziwa Rukwa upande wa kusini-mashariki.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 10,076 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 8,440 [2] walioishi humo.

Tabaka la mwamba linaloenea kutoka upande wa kusini wa Ziwa Rukwa hadi karibu na Ziwa Nyassa linaitwa "Tabaka la Galula" (kwa Kiingereza Galula formation). Ndani ya tabaka hilo visukuku vingi vimepatikana pamoja na mifupa ya dinosauri wawili, Rukwatitan bisepultus[3] na Mnyamawamtuka moyowamkia [4].

  1. https://www.nbs.go.tz, uk 233
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Chunya DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-29.
  3. The basal titanosaurian Rukwatitan bisepultus (Dinosauria, Sauropoda) from the middle Cretaceous Galula Formation, Rukwa Rift Basin, southwestern Tanzania, Eric Gorscak, Patrick M. O'Connor, Nancy J. Stevens & Eric M. Roberts kwenye Journal of Vertebrate Paleontology Volume 34, 2014 - Issue 5
  4. New dinosaur with heart-shaped tail provides evolutionary clues for African continent, tovuti ca Chuo Kikuu cha Ohio, tar 13 Februari 2019
Kata za Wilaya ya Songwe - Mkoa wa Songwe - Tanzania

Chang'ombe | Galula | Gua | Ifwenkenya | Kanga | Kapalala | Magamba | Manda | Mbangala | Mbuyuni | Mkwajuni | Mpona | Mwambani | Namkukwe | Ngwala | Saza | Totowe | Udinde


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Songwe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Galula kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari .
Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno