Dinosauri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Dinosauri
Sanamu ya tiranosauri (Tyrannosaurus rex)
Sanamu ya tiranosauri (Tyrannosaurus rex)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Sauropsida (Wanyama wanaofanana na watambaazi)
Nusungeli: Diapsida (Wanyama wenya mashimo mawili kando la fuyu la kichwa)
Oda ya juu: Dinosauria (Wanyama kama dinosauri)
Ngazi za chini

2 Orders:

  • Ornithischia
  • Saurischia

Dinosauri (kutoka maneno ya Kigiriki δεινός, deinos – "wa kutisha", σαῦρος, sauros - "mjusi"; pia: dinosau, dinosari, dinosaria) ni jina la kundi la reptilia wakubwa sana walioishi duniani miaka milioni kadhaa iliyopita.

Kulinganisha ukubwa wa tiranosauri na binadamu.

Wataalamu huamini ya kwamba dinosauri walitokea miaka milioni 230 iliyopita wakatoweka ghafla miaka 65 iliyopita. Ndege hutazamwa kuwa katika nasaba ya dinosauri.

Ujuzi kuhusu wanyama hao unatokana na visukuku vyao (mabaki ambayo yamekuwa mawe) kama vile mifupa, nyayo, mayai au samadi. Visukuku vya dinosau vimepatikana kwenye mabara yote, hata Antaktika, kwa sababu waliishi wakati mabara yote yalikuwa bado pamoja kama bara kubwa asilia la Pangaia.

Spishi zao

Hadi sasa spishi 500 zimegundulika na idadi ya spishi zilizotambuliwa inazidi kuongezeka.

Kutokana na meno yao imewezekana kutambua chakula chao, kwamba wengine walikuwa wala majani, wengine walanyama.

Wale wakubwa sana walikula majani kama vile apatosauri na brakiosauri na hao walikuwa ndio viumbehai wakubwa kabisa waliowahi kutembea duniani.

Walanyama walikimbia kwa miguu miwili ya nyuma jinsi wanavyofanya watu lakini pia mijusi kadhaa wa leo.

Kulikuwa pia na reptilia wakubwa walioruka hewani walioitwa pterosauri, lakini kinasaba hawakuwa karibu sana na dinosauri.

Wengine wakubwa waliishi baharini kama ikhtiosauri na plesiosauri; hata hao walikuwa kundi lingine.

Picha

Picha zifuatazo zinaonyesha kwanza visukuku vya kweli vya dinosau halafu uchoraji au sanamu zinazoonyesha jinsi gani wataalamu wanadhani mnyama alionekana.

Viungo vya nje

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Crystal Project Babelfish.png Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dinosauri kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Morpho didius Male Dos MHNT.jpg Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dinosauri kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.