Pangaia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ramani ya Pangaia inayoonesha vipande vyake viliovyokuwa mabara ya leo
Mwendo wa mabamba: jinsi Pangaea ilivyoachana na mabara ya leo kutokea

Pangaia (pia: Pangaea kutoka Kigir. πᾶν pan "yote" na γαῖα gaia ardhi, dunia) ni neno la Kigiriki linalomaanisha "dunia yote, dunia nzima".

Katika nadharia ya sayansi ya jiografia inamaanisha bara kubwa linaloaminiwa kuwa liliunganisha bara zote za dunia takriban miaka milioni 250 iliyopita. Maana yake wakati ule sehemu zote za nchi kavu zilikuwepo mahali pamoja kwenye uso wa dunia yetu. Bara hili kuu lilizungukwa na maji ya Panthalassa iliyokuwa bahari ya pekee duniani.

Kuvunjika kwa Pangaia[hariri | hariri chanzo]

Kutokana na mwendo wa gandunia pangaia ilianza kuvunjika takriban miaka milioni 150 iliyopita. Sehemu kubwa 2 zinazoitwa na wataalamu Laurasia na Gondwana zikatokea ambazo zikaendelea kuvunjika tena kwa mabamba ya gandunia ambayo leo hii ni mabara tunavyoijua.

Pangaia ya nadharia ya gandunia[hariri | hariri chanzo]

Katika mawazo ya wataalamu Pangaia haikuwa bara la kwanza duniani; yenyewe ilitokea baada ya kugongana kwa mabara yaliyotangulia. Katika nadharia ya gandunia kila bara liko kwenye bamba la gandunia linaloelea juu ya magma joto ya koti ya dunia. Joto la magma linasukuma mabamba haya na kusababisha mwendo wa mababmba yanaoweza kukaribiana hadi kuungana au kuvunjia na kwenda mbali.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.