Asteroidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
253 Mathilde ni asteroidi yenye vipimo vya 66×48×46 km
Ukanda wa asteroidi katika mfumo wa jua letu

Asteroidi (kutoka Kigiriki ἀστήρ aster = nyota na είδες -eides= ya kufanana) ni gimba la angani linalozunguka jua kama sayari. Ni ndogo kuliko sayari kibete lakini kubwa kushinda kimondo. Mara nyingi huitwa pia "planetoidi" kwa sababu tabia zao zinalingana katika mengi na sayari.

Katika mfumo wa jua letu kuna angalau asteroidi 338,000 zilizotambuliwa hadi leo na wanaastronomia. Nyingi zinazunguka katika ukanda wa asteroidi kati ya njia za Mirihi (Mars) na Mshtarii (Jupiter). Wataalamu hutofautiana kati yao kama hizi ni ama mabaki ya sayari iliyolipuka au vipande vya sayari ambayo haikukamilika bado.

Ukubwa wa asteroidi ni kati ya kipenyo cha kilomita 1,000 hadi sentimita kadhaa.

Tangu mwaka 2006 umoja wa kimataifa wa wanaastronomia umeamua kutofautisha kati ya asteroidi na sayari kibete. Sayari kibete ni gimba mango kubwa lenye masi ya kutosha kufikia umbo la tufe. Kutokana na mapatano haya magimba yaliyohesabiwa kama asteroidi kubwa kama Ceres siku hizi huitwa sayari kibete.

Majina ya asteroidi huwa na na namba mbele na jina linaloweza kupendekezwa na mfumbuzi wake. Asteroidi ya kwanza iliyogunduliwa ilikuwa 1 Ceres. Namba zinatolewa mfululizo na zinaonyesha nafasi yake katika historia ya ufumbuzi wa asteroidi. Leo hii takriban lakhi 2.5 zimepewa majina ya aina hii.

Science-symbol-2.svg Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Asteroidi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.