Ceres

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala hii inamhusu mungu katika dini ya Roma ya Kale. Kwa sayari kibete tazama 1 Ceres

Sanamu ya Ceres katika makumbusho ya Louvre mjini Paris

Ceres aliabudiwa katika ustaarabu wa Roma ya Kale kama mungu wa kike aliyehusika habari za kilimo, rutba na unyumba. Alitazamiwa kama binti wa miungu Saturnus na Ops.

Alilingana na mungu wa Kigiriki Demeter. Katika mitholojia ya Kiroma alizaa watoto wawili na Iupiter.