Santilya
| Kata ya Santilya | |
| Nchi | Tanzania |
|---|---|
| Mkoa | Mbeya |
| Wilaya | Mbeya Vijijini |
| Idadi ya wakazi | |
| - Wakazi kwa ujumla | 17,578 |
Santilya ni kata ya Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Ipo katika tarafa ya Isangati ikiwa na vijiji kama Itizi, Sanje, Jojo, Iswago, Nsheha, Idunda n.k. Imepakana na kata ya Isuto, ikiwa upande wa magharibi, Ilembo upande wa kusini, Igale upande wa mashariki, kaskazini ni wilaya ya Ileje.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 17,624 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 17,578 [2] walioishi humo.
Santilya ni kitovu cha Umalila na wakazi asilia ni hasa Wamalila. Lugha yao ni Kimalila. Kata ya Santilya ina koo kubwa ambazo ni Mwaluanda ambao ni machifu, pia kuna koo kama Mwangwale, Wapyambala, Mwamahonje, Mwasile, Mwasenga, Ngoya n.k. Wamalila ni wakarimu na wachapakazi.
Wakazi wa Santilya wanajihusisha na kilimo cha viazi mviringo na vitamu, maharagwe, mahindi na pareto ambalo ni zao la biashara.
Upande wa elimu Wamalila hawakuwa na mwamko mwanzo ingawa sasa wanaonekana kuja kwa kasi. Kuna shule ya sekondari.
Katika mazingira ya Santilya Jeshi la Wokovu lina wafuasi wengi kiasi.
Msimbo wa posta ni 53211.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2017-03-12.
| Kata za Wilaya ya Mbeya Vijijini – Mkoa wa Mbeya - Tanzania | ||
|---|---|---|
|
Bonde la Songwe | Igale | Igoma | Ihango | Ijombe | Ikukwa | Ilembo | Ilungu | Inyala | Isuto | Itawa | Itewe | Iwiji | Iwindi | Iyunga Mapinduzi | Izyira | Lwanjilo | Maendeleo | Mjele | Masoko | Mshewe | Nsalala | Santilya | Shizuvi | Swaya | Tembela | Ulenje | Utengule/Usongwe | ||
| Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Santilya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |