Iwiji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kata ya Iwiji
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Mbeya Vijijini
Idadi ya wakazi
 - 9,049

Iwiji ni jina la kata ya Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Wakati wa wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 9049[1] walioishi humo. Msimbo wa posta ni 53213.

Kuna vijiji vya Iwiji, Isende na Izumbwe II.

Kijiji cha Izyira[hariri | hariri chanzo]

Kijiji cha Izyira kimepewa hadhi ya kuwa kata inayojitegemea mwaka 2014 ikiwa imetokea baada ya kugawa kata ya Iwiji ambapo mwanzo kijiji hiki kilikuwa kipo kata ya Iwiji. Kijiji hiki kinapakana na kijiji Ibezya cha wilaya ya Ileje kusini mashariki, kusini kinapakana na Wilaya ya Mbozi vijiji vya Hezya na kijiji cha cha Namwangwa na kuendelea mpaka magharibi kijiji cha Haraka na Idiwili kaskazini kuna kijiji cha Iwiji na safu ya milima Mbeye na mlima Makungulu iliyoambatana na msitu Mang'onga na msitu Mbogho.

Misitu hii ni muhimu kwa kuwa ndicho chanzo kikuu cha mito mikuu mitatu ambayo ni Mto Magole, Mto Salaga na Mto Mafumbo. Mito hii ndio chanzo pekee ambayo inashikilia asilimia 85% ya kilimo cha umwangiliaji wa vijiji vyote katika ukanda wa vijiji vyote vilivyovitajwa hapo juu kuwa jirani ya Izyira.

Izyira hukaliwa na makabila matatu ya Wanyiha, Wandali na Wamalila. Kijiji hiki kuna mila na desturi zake kikiongozwa na mila za kijadi. Kiongozi akiitwa mwene wa ukoo wa Mwazembe. Kati ya Wakristo kuna hasa madhehebu yaliyo kwenye jumuiya ya CCT. Kijiji hiki kina shule tatu. Izyira ni shule mama iliyoanzaishwa mnamo miaka ya 1957 kwa mfumo wa shule za TAPA iliyoanza na mwalimu mzawa Winfred Mtindo Mwazembe baadaye zilianzishwa shule mbili kutokana na ongezeko la watu ambazo ni Mwenge na shule ya msingi Masewe. Pia wananchi katika mfumo wa kila kata kujenga shule ya sekondari kijiji kama kijiji walijenga shule ya sekondari ya kijiji kwa mpango wa kijitolea pamoja na kuwa na shule ya sekondari ya kata ambayo ipo makao ya kata pale Iwiji pia mwaka 2009 shule ya sekondari ilifunguliwa katika kijiji cha Izyira mwezi April 29 chini ya mkuu wa shule Godlove Ngonde

Kijiji hiki kinahudumiwa na barabara kuu kutoka mbalizi ikipitia vijiji vifuatavyo mbalizi Izumbwe I, Mganjo, Isangati Santilya, Shipongo, Ilembo, Italazya, Shigamba, Izumbwe II. Iwiji barabara inagawanyika, kushoto inakwenda makao makuu ya Wilaya ya Ileje yaani Itumba na kulia barabara hii ndiyo inakwenda moja kwa moja Izyira hatimaye huendelea Wilaya ya Mbozi kupitia vijiji vya Hezya, ,Nyimbili, Ilengo, Shumba, Hasamba na kuungana tena na barabara kuu ya Dar es Salaam mpaka Zambia pale makao mkuu ya Wilaya ya Vwawa.

Chakula chao kikuu kinatokana na mazao yaani mahindi, ndizi na viazi vitamu. Zao la biashara ni kahawa. Mito mitatu hupitia kijiji hiki, mto Magole upo mashariki sambamba na kijito kidogo kiitwacho Itaga katikati kuna kijito kingine Salaga magharibi kuna mto mkubwa Mafumbo na magharibi kuna kijito kingine shongo. Mito yote hii ndio chanzo kikuu cha uzalishaji wa chakula cha wakazi wa kijiji cha Izyira na vijiji vya jirani mito hii mkubwa miwili yaani Magole na Mafumbo ikisaidiana na vijito hivi hutiririsha maji mwaka mzima. Muungano wa mito hii miwili hufanya mto mmoja unaokwenda kusini kupitia karibu sana na Itumba kuungana na mto Songwe ulio kama mpaka wa Tanzania na Malawi. Kuna milima mkubwa mitatu kaskazini ambayo ni Mlima Mbeye, kaskazini magharibi Mlima Makungulu na magharibi kuna Mlima Mwira. Katika milima hii kuna misitu minene ambayo ndio maji ya mito hii huanzia katika misitu hiyo.

Kutokana na ongezeko la watu misitu hii miaka ya karibuni kumekuwa na uharibifu mkubwa na kusababisha mito hii kupungua sana tena sana kwa ujazo wa maji na kusababisha kupungua kwa kiwango cha unyeshaji wa mvua, kama hatutakuwa na mkakati wa kuzuia uharibifu huu wa misitu hii msitu Mang'onga na msitu Mbogho upo uwezekano wa mito hii kukauka na kusababisha hali mbaya kwa vijiji vyote vinavyopata huduma ya maji ya mito hii mikubwa si IZYIRA tu hata WILAYA jirani kama ILEJE na Mbozi.

Kijiji hiki, pamoja na kuwa na vitongoji kumi vinahudumiwa na zahanati moja tu. Kata ya Izyira ina Jumla ya vijiji vinne ambavyo ni Izyira, Masewe, Inuka na Mapita ikiwa ni kijiji kilichotokea baada ya kugawa kijiji cha Izyira

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya 2012, Mbeya - Mbeya DC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-12.
Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Mbeya VijijiniMkoa wa Mbeya - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bonde la Usongwe | Igale | Igoma | Ihango | Ijombe | Ikukwa | Ilembo (Mbeya vijijini) | Ilungu | Inyala | Isuto | Itawa | Itewe | Iwiji | Iwindi | Iyunga Mapinduzi | Izyira | Lwanjiro | Maendeleo | Mjele | Masoko | Mshewe | Nsalala | Santilya | Shizuvi | Swaya | Tembela | Ulenje | Utengule Usongwe


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iwiji kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.