Wamalila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wamalila ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi hasa katika Mkoa wa Mbeya, Wilaya ya Mbeya Vijijini, kata za Isuto, Ilembo, Iwiji, Masoko, Santilya, Iyunga Mapinduzi, bonde la Mbalizi na nyingine pia.

Lugha yao ni Kimalila, mojawapo ya lugha za Kibantu, ambayo inafanana sana na Kisafwa na Kinyiha kwa sarufi na maneno, na kutofautiana kwa baadhi ya matamshi na lafudhi.

Eneo la Umalila[hariri | hariri chanzo]

Umalila iko kusini kutokea Mbalizi katika nyanda za juu kwenye mazingira ya Bonde la Umalila. Hata hivyo hali ya hewa ni ya baridi sana miezi ya sita hadi nane.

Umalila ni bonde linalopakana na maeneo ya makabila kadhaa kama Wanyiha upande wa magharibi, Wasafwa upande wa kaskazini, Wandali upande wa kusini na Wanyakyusa upande wa mashariki.

Mito ya Songwe ya kusini na Songwe ya kaskazini ina chanzo katika Umalila.

Ardhi ina rutuba ya kutosha, hivo huzalisha nafaka za kutosha hasa mahindi, maharage, na vyakula vingine kama viazi mviringo na viazi vitamu, lakini mazao ya biashara ni kahawa na pareto.

Koo za Wamalila[hariri | hariri chanzo]

Wamalila kwa ujumla wanakadiriwa kufikia 120,000 wanaolizunguka bonde hili kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012. Kama ilivyo kawaida ya makabila yote, pia kabila hili lina koo kubwa zenye watu wengi: baadhi ni kama ukoo wa Mwampamba, ambao ndio machifu wa kabila hili na wanapatikana maeneo ya Santilya, Jojo, Ilembo, Isuto, Nsheha na maeneo mengi ya Umalila, halafu Mwahalende, wanaopatikana Ilembo, Masoko, Ikupula na Iyunga; pia koo za Mwasenga, Mwambwiga, Mzumbwe, Mwaluvanda, Mwasile, Mwashibanda, Mboya, Mwaigaga, Mwangwale, Mwampepu, Mwazembe ambao umegawanyika kwenye koo kama Mbeye, Nambeye na Simbeye, Mwalyanzi, Mpunji, Mwalukalanje, Mboma, Mwanjoka, Hansuli na nyingine nyingi.

Ukoo mwingine ya Wamalila ni ha0nga ambao wamegawa nyika katika koo kama Mwasenga, Lyala, Ntali, Shimunya na koo za Sikaonga, Shamaonga, Kyawonga n.k. na koo zilizopo Malawi, Zambia na Msumbiji. Ukoo huu ukienda kwa Wanyiha, Wanyamwanga, Walambya (Songwe) hudai ni ukoo mwenzao, lakini si hivyo tu: ukoo huu umejitanua sana sehemu zà Morogoro, Songwe, Tanga, Zambia na Malawi lakini kwao au asili yao ni kijiji cha Iwala-Itale-Umalila, hivyo watu hao ni Wamalila.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamalila kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.