Wasegeju

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wasegeju ni kabila la watu kutoka eneo baina ya Tanga na mpaka wa Kenya, pwani ya nchi ya Tanzania. Kabila hili lina mahusiano mengi na Wadhaiso. Mwaka 2003 idadi ya Wasegeju ilikadiriwa kuwa chini ya 15,000, na chini ya 7,000 tu ndio wanaosema Kisegeju [1]. Wasemaji wa lugha hiyo wanapatikana katika vijiji vya Daluni na Bwiti, lakini pia Wasegeju wa maeneo ya Boma kwenye mwambao wanaongea lugha ambayo wanayoisibu Kisegeju lakini ni tofauti sana na hicho Kisegeju cha Usambaani ama kwa neno lingine Kidhaisu.

Asili ya kabila hilo inasemekana kuwa limeanzia katika pembe ya Afrika ambapo miaka mingi iliyopita watu hawa walihama kwenye makazi yao kwa sababu mbalimbali, zikiwemo biashara, ufugaji na vita.

Nyaraka za Wareno zinaonyesha kwamba hii jamii walikuwa wafugaji na wapiganaji vita. Wasegeju wanajulikana sana kwenye mapisi ya jamii za mwambao kwa sababu ya vita vyao na Wazimba.

Vilevile inasemekana kuwa mwanzo kabila hili halikujulikana kama "Wasegeju" bali kutokana na kuhama kwao na kueleka juu ndipo watu wakasema "Wasogea juu" na hapo likapatikana jina la "Wasegeju".

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wasegeju kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.