Nenda kwa yaliyomo

Waburunge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Barabara katika wilaya ya Kondoa linakopatikana kabila la Waburunge

Waburunge ni kabila la watu wa Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Dodoma, Wilaya ya Kondoa. Lugha yao ni Kiburunge, mojawapo ya lugha za Kikushi.

Waburunge kwa idadi ni wachache sana (300,000 hivi) na wanapatikana katika tarafa za Goima na Mondo, pia wachache wapo katika kata za Gwandi, Kondoa Mjini. Sasa hivi wanakaa kila kona ya Tanzania na wanapenda kushirikiana na watu wa makabila tofauti.

Lugha yao si ya Kibantu ila ina uhusiano kidogo na lugha za Wairaqw na Wagorowa kwani Mburunge anaweza kuelewa Mwiraq anachokiongea kutokana na maneno yao kuwa na mizizi ileile bali viambishi tofauti.

Utamaduni wao

[hariri | hariri chanzo]

Waburunge wana tamaduni zifuatazo wanazoziheshimu sana hadi leo:
1. kiongozi mkuu wa hili kabila ni mzee na ana baraza lake la wazee
2. wanarithi wajane, ila si wote
3. wanaume wanatahiriwa porini na wanakaa huko kwa zaidi ya miezi sita; wakati wa kutolewa hufanyiwa sherehe ya ngoma ambayo inaitwa "choraa" kwa mchana na usiku vijana waliokuja kwa ajili ya ngoma hucheza na kukesha ngoma inaitwa goroisoo' na akina mama hucheza "slasla/aso" na ngoma hizo huambatana na pombe pamoja na nyama
4. kwao mwanamke hausikii sana kwenye mambo ya maendeleo
5. katika suala la ndoa mwanamke anaweza kuozeshwa hata kwa mtu asiyemjua wala kumuona hata siku moja, kwani anasikiliza anachoambiwa na wazazi wake
6. kuhusu dini wengi wameanza kujiunga nazo: robo ya Waburunge ni Wapagani bali wengine wamejiunga na Ukristo na wachache sana wapo katika Uislamu
7. suala la elimu kwao ni si kipaumbele sana, kwani huona kumpeleka mtoto shule ni sawa na kupoteza muda
8. wana ngoma zao za asili na wanaziheshimu sana kwani kila mtu anachezeshwa kutokana na jinsia yake na kanuni za ukoo lakini kila mtu lazima acheze kwa mwaka; ngoma yao kuu hufanyika mwezi wa saba kuanzia tarehe saba hadi kumi katika kijiji cha Chambalo
9. wanaamini pombe ni kitu muhimu kwani katika shughuli zozote za mkusanyiko lazima pombe iwepo. pombe yao ya asili ni pombe ya udo inayotokana na mtama mwekundu na pombe ya asali(kangara), pombe hizo ndizo hutumika kwenye mila na ngoma zote za asili za waburunge
10. wanafuga,kuwinda na kurina asali pia
11. wanapenda kukaa milimani sana
12. wana njia zao za asili za kutambua majira ya mwaka na jinsi mwaka utakavyokuwa kama utakuwa na mvua nyingi au kidogo
13. wana njia za asili za kuhifadhi vyakula
14. wana nyumba zao za asili ambazo zinajengwa kwa miti na udongo
15. ni watu wakarimu sana na wana moyo wa upendo kama ukijua jinsi ya kuishi nao[watii na pia ni wakorofi sana
16.waburunge kwa asili ni watu wachapakazi sana, kwani kijana wa kiburunge hufundishwa umahiri wa kazi akiwa jandoni
17. watani wao ni Wasukuma, Wanyiramba, Wagogo na Wakaguru

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waburunge kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.