Kondoa (mji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kondoa Mjini)
Jump to navigation Jump to search
Kondoa mjini
Kondoa-Mjini.jpg
Kondoa mjini is located in Tanzania
Kondoa mjini
Kondoa mjini
Mahali pa Kondoa katika Tanzania
Majiranukta: 4°54′0″S 35°46′12″E / 4.9°S 35.77°E / -4.9; 35.77
Nchi Tanzania
Mkoa Dodoma
Wilaya Kondoa
Idadi ya wakazi
 - 21,878

Kondoa ni mji mdogo katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania na makao makuu wa Wilaya ya Kondoa yenye postikodi namba 41701[1] . Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Kondoa Mjini ilikuwa na wakazi wapatao 14,382 [2] waishio humo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo vya mji ilikuwa kituo cha biashara kwenye njia ya misafara katika karne ya 19 na wakati wa kufika kwa Wajerumani 1891 kulikuwa na boma la wafanyabiashara Waarabu. Msikiti wa kwanza ulijengwa mwaka 1885. [3]

Wakati wa ukoloni wa Kijerumani mji ulijulikana kwa jina Kondoa-Irangi ukawa kituo cha jeshi la kikoloni la Kijerumani.

Mwaka 1912 ilikuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Kondoa-Irangi.

Mwaka 1910, kanisa la kwanza lilijengwa.

Kuanzia mwaka 2011 Kondoa ni makao makuu ya jimbo jipya la Kanisa Katoliki, linaloongozwa na askofu Bernardin Mfumbusa.

Ndani ya wilaya ya Kondoa kuna vijiji zaidi ya 180.

Makabila makuu ni Warangi, Wasandawe, Waburunge na Wasi.


Baadhi ya vijiji vya kata ya Kondoa Mjini vyenye shule ya msingi ni Kondoa yenyewe, Iboni, Ubembeni, Miningani na Mpalangwi. Takriban asilimia 60 za wakazi wa kata ya Kondoa Mjini ni Warangi.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Kondoa - Mkoa wa Dodoma - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bereko | Bolisa | Bumbuta | Busi | Changaa | Chemchem | Haubi | Hondomairo | Itaswi | Itololo | Kalamba | Kikilo | Kikore | Kilimani | Kingale | Kinyasi | Kisese | Kolo | Kondoa Mjini | Kwadelo | Masange | Mnenia | Pahi | Salanka | Serya | Soera | Suruke | Thawi|


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kondoa (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.