Kondoa (mji)
Kondoa mjini | |
Mahali pa Kondoa katika Tanzania |
|
Majiranukta: 4°54′0″S 35°46′12″E / 4.90000°S 35.77000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Dodoma |
Wilaya | Kondoa |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 26,179 |
Kondoa ni mji mdogo katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania na makao makuu wa Wilaya ya Kondoa Vijijini yenye postikodi namba 41701[1].
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 26,179 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Kondoa Mjini ilikuwa na wakazi wapatao 14,382 [3] waishio humo.
Takriban asilimia 60 za wakazi wa kata ya Kondoa Mjini ni Warangi.
Mji huo una takriban asilimia 70 ya Waislamu na asilimia 30 ya Wakristo, huku dini za asili zikiwa karibu zimepotea kabisa. Mahusiano kati ya makundi ya dini ni mazuri.
Ndani ya wilaya ya Kondoa kuna vijiji zaidi ya 180. Makabila makuu ni Warangi, Wasandawe, Waburunge na Wasi.
Baadhi ya vijiji vya kata ya Kondoa Mjini vyenye shule ya msingi ni Kondoa yenyewe, Iboni, Ubembeni, Miningani na Mpalangwi.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Chanzo cha mji kilikuwa kituo cha biashara kwenye njia ya misafara katika karne ya 19 na wakati wa kufika kwa Wajerumani mwaka 1891 kulikuwa na boma la wafanyabiashara Waarabu. Msikiti wa kwanza ulijengwa mwaka 1885. [4]
Wakati wa ukoloni wa Kijerumani mji ulijulikana kwa jina la Kondoa-Irangi ukawa kituo cha jeshi la kikoloni la Kijerumani.
Mwaka 1912 ilikuwa makao makuu ya mkoa mpya wa Kondoa-Irangi.
Mwaka 1910, kanisa la kwanza lilijengwa.
Kuanzia mwaka 2011 Kondoa ni makao makuu ya jimbo jipya la Kanisa Katoliki, linaloongozwa na askofu Bernardin Mfumbusa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2020-03-21. Iliwekwa mnamo 2017-10-08.
- ↑ https://www.nbs.go.tz
- ↑ "Sensa ya 2012, Dodoma - Kondoa DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2016-05-18.
- ↑ Makala "Kilossa" na "Kondoa-Irangi" katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani
Kata za Wilaya ya Kondoa Mjini - Mkoa wa Dodoma - Tanzania | ||
---|---|---|
Bolisa | Chemchem | Kilimani | Kingale | Kolo | Kondoa Mjini | Serya | Suruke |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dodoma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kondoa (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |