Wayao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kinyago, Malawi

Wayao ni kabila la Kibantu kutoka eneo la karibu na Ziwa Nyasa.

Mwaka 2001 idadi ya Wayao ilikadiriwa kuwa 1,942,000, ambao kati yao 1,000,000 wanaishi Malawi, 450,000 ni wakazi wa Msumbiji, na 492,000 wako Tanzania [1].

Wayao ni miongoni mwa wabantu wanaopatikana mataifa kadhaa barani Afrika.

Wengi wa wayao ni wanaabudu dini ya kiislamu na kwa ujumla wao wameenea kwenye mataifa ya Malawi, Msumbiji, na Tanzania katika mikioa ya mtwara na Ruvuma.

Wanasifika sana kwa kuwa na utambulisho wenye nguvu wa kiutamaduni unaovuka mipaka.

shughuli yao kubwa ni kilimo cha hapa na pale, Kihistoria wakati waarabu walipokuwa wakiwasili pwani ya afrika walianza kufanya biashara na wayao katika bidhaa za pembe za ndovu, watumwa kwa kubadilishana nguo na bunduki.

kwa sababu maeneo ya kibiashara walikuja kuwa matajiri na kuwa kabila linalovutia barani Afrika.

kukua kwa kabila la Wayao kulikuja baada ya kuchukua kwa mkoa wa niassa huko msumbiji katika karne ya 19, tangu hapo wayao walianza kuondoka katika makazi yao ya kiutamaduni ambayo ni yalikuwa Malawi na tanzania hali iliyopelekea kusambaa kwa kabila hilo nchini.

baada ya vita ya kwanza ya dunia katika karne ya 20 kabila la wayao lilijikita katika dini ya uislamu kufuatia biashara iliyokuwepo kati ya waswahili na waarabu ambapo machifu walihitaji wenyeji waliokuwa na uwezo wa kusoma na kuandika.

waalimu wa kiislamu walioajiriwa kuishi katika vijiji vya wayao walifanikiwa kueneza dini yao kupitia mafunzo mbalimbali waliyowapa wayao ikiwemo elimu, vitabu vya dini, mavazi ya dini ya kiislamu na nyumba zenye pembe badala ya zile za mduara.

hata hivyo kiongozi wa wayao alipambana kwa nguvu zote ukoloni wa Wareno, Waingereza na wajerumani lakini pia utawala wowote wa kikoloni ambao ulionekana ni tishio kwa uchumi wake.

chifu wa wayao Mataka aliupinga Ukristo kwani waislamu waliwapa mahitaji yao ya kijamii ambayo yaliwafaa kwa tamaduni zao, kwa sababu siasa na ibada ya utawala wa Machifu, uongofu wao kwa Uislamu ulisababishwa masomo yao kufanya hivyo hivyo.

Tuwatizame wayao wa Msumbiji.

walikuwa wakiishi kaskazini mwa taifa hilo lililotawaliwa na wareno, ukiangalia   kwa ukaribu historia ya wayao wa msumbiji katika jografia yao ipo katika kijiji kidogo cha Chiconono, katika jimbo kaskazini magharibi mwa Msumbiji la Niassa.

Nao ni wakulima wa hapa na pale ingawaje vilevile walikuwa wamejikita kwenye uuzaji biashara ya pembe za ndovu na biashara ya watumwa.

Walikumbwa na anguko la kisiasa na kiuchumi baada ya wareno kufika katika jimbo la Niasa ambako walianzisha kampuni ambapo walijenga makazi na kuvunja mashamba na kuharibu  biashara  na kubadilirisha kuwa uchumi nauchumi unaotegemea mazao uliokuwa ukichungwa na wareno.

Kupanuka kwa himaya ya Kireno kulianzisha kituo muhimu cha biashara, ngome ya jeshi, na bandari tangu karne ya 15 kiasi cha kuwavutia majeshi ya waislam  wakiwamo wasomali, waswahili.

Misafara ya wareno na uenezwaji wa dini ya kikristo ndio kuliwafanya zaidi wareno kujitanua ingawaje baadae karne ya 19 wareno walikuja kujihusisha na biashara ya utumwa kutoka msumbiji hadi brazil.

Himaya ya wareno kwa wakati huo lilikuwa tawala kubwa kisiasa na kiuchumu duniani, kwa wakati huo walikuwa wakiendesha kilimo kilichopata mafanikio kwa kuwalipa makundi makubwa ya wakulima ya makabila, na katika kundi la wayao uzalishaji wao ulikuwa chini uongozi wa wareno.

Ingawaje wayao walikuwa wanaenzi mila na tamaduni zao namna ya kilimo chao cha hapa na pale, kama waisali wayao hawakuzisiamamia na kujikuta wameanza kufunzwa elimu ya ukristo, na kuanza kufundisha rugha ya kireno kwa waislamu.

Kwa sasa, wayao wanakadiliwa kufikia 450,000 wanaishi msumbiji, ambao ni asilimia 40 ya wakazi wa Lichinga.

Wayao Nje ya Msumbiji

Miaka ya 1830 wayao wakiwa kama wafanyabishara na wakulima walianza kuenea eneo la mashariki mwa malawi, ambao walikuwa matajiri katika mila na muziki ambao wengi wao walikuwa waislamu.

Wayao walikuwa na mahusiano ya karibu na Kiswahili katika pwani wakati wa karne ya 19, na kukubaliwa baadhi ya maeneo ya utamaduni wao, kama vile usanifu na Uislamu, miongoni mwao waliopata umaarufu mkubwa ni pamoja na marais wawili wa zamani wa Malawi Bakili Muruzi pamoja na Joyce Banda.

wayao walikuwa na uhusiano wa Karibu na waswahili wa pwani katika karne ya 19 na kuiga baadhi ya Tamaduni zao ikiwamo  usanifu na Uislamu ingawaje waliendelea utamaduni wao wakitaifa.

Ushirikiano wao na waarabu uliwapa fursa ya upatikanaji wa silaha za moto ambazo walizitumia katika vita baina yao na wangonina Chewa, Wayao walikuwa wapinzani wa tawala la kijerumani la kusini mwa afrika  katika eneo la tanzania Rwanda na Burundi.

Kwa Upande wa Rugha wayao wenyewe wanaongea Rugha Inaitwa Kiyao

na wanakadiliwa kufikia milioni moja huko Nchini Malawin karibu laki tano katika taifa la Msumbiji na humu Nchini kulingana wavuti wanafikia laki nne tisini na mbili elfu.

Wakipatikana zaidi katika eneo kati ya Ruvuma na karibu na mto Lugenda kaskazini mwa msumbiji vilevile wanazungumza rugha Rasmi ikiwamo Kiswahili kwa wale waliopo tanzania, kiingereza kwa wale wa Malawi na Humu Nchini na kireno wanazungumza wale waliopo Nchini Msumbiji

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wayao kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.