Wayao (Tanzania)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kinyago, Malawi

Wayao ni kabila la Kibantu kutoka eneo la karibu na Ziwa Nyasa.

Mwaka 2001 idadi ya Wayao ilikadiriwa kuwa 1,942,000, ambao kati yao 1,000,000 wanaishi Malawi, 450,000 ni wakazi wa Msumbiji, na 492,000 wako Tanzania [1]

Wayao ni miongoni mwa Wabantu wanaopatikana katika mataifa kadhaa barani Afrika na kwa ujumla wao wameenea Malawi, Msumbiji na Tanzania katika mikoa ya Mtwara na Ruvuma.

Wakipatikana zaidi katika eneo kati ya Ruvuma na karibu na mto Lugenda kaskazini mwa Msumbiji.

Wanasifika sana kwa kuwa na utambulisho wenye nguvu wa kiutamaduni unaovuka mipaka.

Shughuli yao kubwa ni kilimo cha hapa na pale.

Upande wa lugha Wayao wenyewe wanaongea Kiyao; vilevile wanazungumza lugha rasmi ikiwamo ile ya Kiswahili kwa wale waliopo Tanzania, Kiingereza kwa wale wa Malawi na Tanzania na Kireno kwa wale waliopo nchini Msumbiji.

Wengi wao ni waumini wa dini ya Uislamu.

Miongoni mwao waliopata umaarufu mkubwa ni pamoja na marais wawili wa zamani wa Malawi: Bakili Muruzi pamoja na Joyce Banda.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Waarabu walipokuwa wakiwasili pwani ya Afrika walianza kufanya biashara na Wayao kwa kubadilishana nguo na bunduki na bidhaa za pembe za ndovu na watumwa; hivyo walikuja kuwa matajiri na kuwa kabila linalovutia barani Afrika.

Kukua kwa kabila la Wayao kulikuja baada ya kuchukua kwa mkoa wa Niassa huko Msumbiji katika karne ya 19. Tangu hapo Wayao walianza kuondoka katika makazi yao ya kiutamaduni, ambayo yalikuwa Malawi na Tanzania ya leo, hali iliyopelekea kusambaa kwa kabila hilo nchini.

Baada ya vita vya kwanza vya dunia katika karne ya 20 kabila la wayao lilijikita katika dini ya Uislamu kufuatia biashara iliyokuwepo kati ya Waswahili na Waarabu ambapo machifu walihitaji wenyeji wenye uwezo wa kusoma na kuandika.

Waalimu wa Kiislamu walioajiriwa kuishi katika vijiji vya Wayao walifanikiwa kueneza dini yao kupitia mafunzo mbalimbali waliyowapa Wayao ikiwemo elimu, vitabu vya dini, mavazi ya dini ya Kiislamu na nyumba zenye pembe badala ya zile za mduara.

Hata hivyo kiongozi wa Wayao alipambana kwa nguvu zote na ukoloni wa Wareno, Waingereza na Wajerumani lakini pia utawala wowote wa kikoloni ambao ulionekana ni tishio kwa uchumi wake.

Chifu wa Wayao Mataka aliupinga Ukristo kwani Waislamu waliwapa mahitaji yao ya kijamii ambayo yaliwafaa kwa tamaduni zao, kwa sababu siasa na ibada ya utawala wa machifu, uongofu wao kwa Uislamu ulisababishwa masomo yao kufanya Vivyo hivyo.

Wayao wa Msumbiji[hariri | hariri chanzo]

Walikuwa wakiishi kaskazini mwa taifa hilo lililotawaliwa na Wareno. Ukiangalia kwa ukaribu historia ya Wayao wa Msumbiji katika jiografia yao ipo katika kijiji kidogo cha Chiconono, katika jimbo la Niassa, kaskazini magharibi mwa Msumbiji.

Nao ni wakulima wa hapa na pale ingawaje vilevile walikuwa wamejikita kwenye uuzaji biashara ya pembe za ndovu na biashara ya watumwa.

Walikumbwa na anguko la kisiasa na kiuchumi baada ya Wareno kufika katika jimbo la Niassa ambako walianzisha kampuni ambapo walijenga makazi na kuvunja mashamba na kuharibu biashara na kubadilisha kuwa uchumi unaotegemea mazao uliokuwa ukichungwa na Wareno.

Kupanuka kwa himaya ya Kireno kulianzisha kituo muhimu cha biashara, ngome ya jeshi, na bandari tangu karne ya 15 kiasi cha kuwavutia majeshi ya Waislamu, wakiwamo Wasomali na Waswahili.

Misafara ya Wareno na uenezwaji wa dini ya Ukristo ndio kuliwafanya zaidi Wareno kujitanua ingawaje baadaye (karne ya 19) Wareno walikuja kujihusisha na biashara ya utumwa kutoka Msumbiji hadi Brazil.

Himaya ya Wareno kwa wakati huo ilikuwa tawala kubwa kisiasa na kiuchumu duniani, kwa wakati huo walikuwa wakiendesha kilimo kilichopata mafanikio kwa kuwalipa makundi makubwa ya wakulima ya makabila, na katika kundi la Wayao uzalishaji wao ulikuwa chini ya uongozi wa Wareno.

Ingawaje Wayao walikuwa wanaenzi mila na tamaduni zao, namna ya kilimo chao cha hapa na pale, kama waisali Wayao hawakuzisimamia na kujikuta wameanza kufunzwa elimu ya Ukristo, na kuanza kufundisha lugha ya Kireno kwa Waislamu.

Kwa sasa, Wayao wanaoishi Msumbiji wanakadiriwa kufikia 450,000, ambao ni asilimia 40 za wakazi wa Lichinga.

Wayao nje ya Msumbiji[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya 1830 Wayao, wakiwa wafanyabiashara na wakulima, walianza kuenea mashariki mwa Malawi, ambako walikuwa matajiri katika mila na muziki ambao wengi wao walikuwa Waislamu.

Wayao walikuwa na mahusiano ya karibu na Uswahili katika pwani wakati wa karne ya 19, na kukubaliwa baadhi ya maeneo ya utamaduni wao, kama vile usanifu na Uislamu.

Wayao walikuwa na uhusiano wa karibu na Waswahili wa pwani katika karne ya 19 na kuiga baadhi ya tamaduni zao, ikiwamo usanifu na Uislamu, ingawaje waliendelea utamaduni wao wa kitaifa.

Ushirikiano wao na Waarabu uliwapa fursa ya kupata silaha za moto ambazo walizitumia katika vita baina yao na Wangoni na Wachewa. Wayao walikuwa wapinzani wa utawala wa Wajerumani kusini mwa Afrika katika eneo la Tanzania, Rwanda na Burundi za leo.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. [1].
Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wayao (Tanzania) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.