Wagweno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wagweno ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Kilimanjaro, upande wa Kaskazini wa Milima ya Upare. Lugha yao ni Kigweno.inasemekana asiliyao wametoka maeneo ya Taita na Voi nchini kenya.kiasili wagweno ni katika jamii zilizo toka habeshi ya kale na ndio maana ukiangalia kwa makini tamaduni zao utaona kwamba hazifanani sana na wabantu bali na wahamitiki.tazama hata katika ngoma ya kigweno ambayo wanaiita mrangi[mwanzi]hawatumii ngoma kama wa Bantu.

SABABU YA WAO KUKIMBIA KENYA NA KUHAMIA TANZANIA YA LEO[hariri | hariri chanzo]

Kilicho wakimbiza huko kenya ya kale na kuhamia eneo linalojulikana kama milima ya ugweno kwa sasa ni vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Taita na Voi.lakini kuna nadharia moja inayosema kwamba kabla wagweno hawajahamia rasmi katika milima hiyo ya upare walituma wapelelezi kwanza;walifika eneo husika na kisha wakaerudisha taarifa yao wakasema;Mringa ua khona[yaani mito ya huko inatoa sauti katika kutiririka kwake na hapo jina ugweno likazaliwa yaani kughona ni muungurumo.kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwamba mgweno ni yeyote aliye kuja na kufanya makazi yake katika milima hiyo ya uzuri ya ugweno.kwa hiyo ndio kusema kwamba wahenga walitoka Taita,voi,uchagani,na hata upareni ndio maana unaweza kukuta hata koo za wasangi,wanzava,nk.mfano mzuri ni mzee modongo na wenzake ambao waliitwa na wasuya kutoka usangi ili kuja kuzuia vita visiingie ugweno ukoo huu mpaka leo unapatikana maeneo ya Chanjale kwa mkuti njia ya kwenda mangio na vuchama na kuna mzee maarufu wa ukoo huo aitwae kiogwe msangi ambaye alifariki dunia mwaka 1995.

MILA NA DESTURI ZA WAGWENO[hariri | hariri chanzo]

Kwa asili wagweno hapo kale walikuwa wapagani wanao abudu mungu jua [RUBHA]Pamwe na mwandani wake MWIRI[MWEZI]Mkewe jua sanjari na watoto wao nyota.ibada hii ya kuelekea jua iliambatana na uabudu wa mizimu.na ndio maana kuhani wa kigweno alipo chinja mnyama na kumchuna ngozi yake aliweza kutazama maini[kupiga ramli kwa kutumia viungo kwemye tumbo la mnyama.tena wanyama hawa walichinjwa kwenye eneo maalumu liitwalo kwa kigweno ngondinyi.mara nyingi eneo hili walihusika wanaume bighairi wanawake kwasababu kwa mila ya kigweno wanaume ndio makuhani.mara nyingi katika eneo la kuzunguka ngondinyi kulipandwa mimea maalum iitwayo Mathale,ambayo kwa mujibu wa mapokeo ya wagweno ni mimea mitakatifu.mnyama anapo chinjwa kuhani hukata vipande vidogo vidogo na kuviweka eneo husika kisha huchukua pombe ima mbege au dDengelua kisha ata tazama mbinguni mkononi ameshika pombe kamba ishara ya tambiko na kusema RUBHA KAGHU NGOMA MBAI;yaa naamini mungu yuko juu lakini chini kuna mizimu kisha humwaga pombe na kusema anacho kusudia,kama anataka mvua inyeshe au anakusudia kuondosha MSINYANYO[mkosi.kwa maana kwa mujibu wa mapokeo ya wagweno mkosi kwao lilikuwa jambo kubwa sana na ndio maana hata mtoto aliye zaliwa na ulemavu wa aina yeyote alitolewa kafara kwenye jiwe la watoto kwa kigweno IGHWE YA BHANA.mhanga alikuwa anachukuliwa kwenye jiwe husika mamaye humbembeleza akiisha kulala hulazwa kwenye kilele cha jiwe na anapo amka ghafla huporomoka na kufa na watakua wameondoa mkosi katika jamii na kumfurahisha mahoka.

kuna kisa kimoja cha kale juu ya bwana mkubwa mmoja aliyeitwa Kindobhai wakati anafukuzwa na maadui kunako eneo ambalo kwa sasa kuna hifadhi ya wanyama ya Tsavo karibia na ziwa jipe ina semekana alipiga fimbo yake kwenye maji na yeye mifugo na wafuasi wake wakavuka salama!masimulizi juu ya wagweno ni mengi sana kiasi kwamba msomaji unaweza ukastaajabu mpaka leo kuna mawe ya ajabu ambayo yako mithili ya watu;inasemekana maadui hapo kale walikuwa wanakuja kuiba mifugo huko lakini kulingana na ujzi wa wazee wakageuzwa mawe kwa njia ya miujiza.