Voi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Voi ni mji wa Kusini mwa Kenya uliopo kwenye njiapanda ya njia za reli pia barabara za Mombasa-Nairobi Taveta. Idadi ya wakazi ni takriban 33,000. Uko kando ya vilima vya Voi.

Ni sehemu ya wilaya ya Taita-Taveta kwenye Mkoa wa Pwani.

Uchumi wa mji hutegemea kilimo na utalii. Kuna mashamba makubwa ya katani katika mazingira ya mji.

Mji uko kando ya mbuga ya wanayama ya Tsavo.

Chanzo cha mji kilitokea kabla ya ukoloni wakati chifu kutoka Ukambani aliyeitwa Kivoi alianzaisha kituo cha misafara ya biashara ya watumwa kwenda Mombasa. Mji wa kisasa ulianzishwa mara baada ya kufika kwa reli ya Uganda kutoka Mombasa mwaka 1898.