Kisumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kisumu
Skyline ya Kisumu
Kisumu is located in Kenya
<div style="position: absolute; z-index: 2; top: Expression error: Unexpected < operator.%; left: Expression error: Unexpected < operator.%; height: 0; width: 0; margin: 0; padding: 0;">
Kisumu
Kisumu
Mahali pa mji wa Kisumu katika Kenya
Viwianishi: 0°6′S 34°45′E / 0.1°S 34.75°E / -0.1; 34.75
Nchi Bendera ya Kenya Kenya
Mikoa Mkoa wa Nyanza
Wilaya Wilaya ya Kisumu
Idadi ya wakazi
 - 968,909
Kitovu cha Kisumu

Kisumu ni mji mkubwa wa tatu wa Kenya, ukiwa na wakazi 968,909 (2009). pia mji mkubwa wa Kenya ya Magharibi na makao makuu ya kaunti ya Kisumu.

Mji uko kando ya ziwa Viktoria Nyanza, una bandari kubwa ya nchi katika ziwa hilo. Mji na bandari vilianzishwa kwa jina la "Port Florence" mwaka 1901 wakati reli ya Uganda ilipofika huko kutoka Mombasa.

Kuna feri ziwani kutoka Kisumu kwenda Mwanza, Bukoba, Entebbe, Port Bell na Jinja.

Kiuchumi Kisumu ina viwanda kadhaa, hasa vya sukari, samaki, vitambaa, pia ya bia.

Maendeleo ya Kisumu yalikwama miaka mingi kwa sababu kwa miaka mingi Wajaluo walisimama upande wa upinzani wa kisiasa, hivyo serikali haikupeleka miradi tena katika eneo hilo.