Kaunti ya Nyeri
Kaunti ya Nyeri | |
---|---|
Kaunti | |
Kilele cha Lenana katika Mlima Kenya, Kaunti ya Nyeri | |
Kaulimbiu: "" | |
![]() Kaunti ya Nyeri katika Kenya | |
Nchi | ![]() |
Nambari | 19 |
Ilianzishwa | Tarehe 4 Machi, 2013 |
Ilitanguliwa na | Mkoa wa Kati |
Mji mkuu | Nyeri |
Miji mingine | Karatina, Othaya, Kiganjo |
Serikali | |
Gavana | Edward Mutahi Kahiga |
Seneta | Ephraim Maina |
Mwakilishi wa wanawake | Rahab Mukami Wachira |
Bunge | Bunge la Kaunti ya Nyeri |
Maeneo bunge | |
Eneo | |
Jumla | km2 3 325 (sq mi 1 284) |
Idadi ya Watu | |
Jumla | 759,164 |
Msongamano | 228 /km² |
Majira ya Saa | Saa za Afrika Mashariki (UTC+3) |
Tovuti nyeri.go.ke |
Kaunti ya Nyeri ni mojawapo ya kaunti 47 za Kenya, iliyoko katika eneo la Kati, kwenye miteremko ya magharibi ya Mlima Kenya. Inapakana na Kaunti ya Laikipia kaskazini, Kaunti ya Nyandarua magharibi, Kaunti ya Murang'a kusini, na Kaunti ya Kirinyaga mashariki. Ina idadi ya watu takriban 759,164 kulingana na sensa ya mwaka 2019[1]. Mji wake mkuu na mkubwa ni Nyeri. Nyeri imegawanyika katika maeneo bunge 6: "Tetu, Kieni, Mathira, Othaya, Mukurweini, na Nyeri Mjini". Inajulikana kwa mandhari ya milima, bustani za kahawa na chai, utalii wa asili karibu na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kenya, pamoja na kuwa eneo la kihistoria la makazi ya Lord Robert Baden-Powell, mwanzilishi wa harakati ya Skauti duniani.
Jiografia
[hariri | hariri chanzo]Kaunti ya Nyeri imepakana na Laikipia (kaskazini), Kirinyaga (mashariki), Murang'a (kusini) na Nyandarua (magharibi).
Topografia ya kaunti huwa na miinuko mikali na mabonde. Mlima Kenya hupatikana katika mpaka wa Meru na Nyeri. Mto Chania na Mto Sagana ndiyo mito mikubwa ambayo hupitia katika kaunti hii[2].
Utawala
[hariri | hariri chanzo]Kaunti ya Nyeri imegawanyika ifuatavyo[3]:
Eneo bunge/kaunti ndogo | Kata |
---|---|
Tetu | Dedan Kimathi, Wamagana, Aguthi-Gaaki |
Kieni | Mweiga, Naromoro, Kiamathaga, Mwiyogo/Endarasha, Mugunda, Gatarakwa, Thegu River, Kabaru, Gakwa |
Mathira | Ruguru, Magutu, Iriaini, Konyu, Kirimukuyu, Karatina Town |
Othaya | Mahiga, Iria-ini, Chinga, Karima |
Mukurweini | Gikondi, Rugi, Mukurwe-ini West, Mukurwe-ini Central |
Nyeri Town | Kiganjo/Mathari, Rware, Gatitu/Muruguru, Ruring'u, Kamakwa/Mukaro |
Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [4]
[hariri | hariri chanzo]- Tetu 80,453
- Kieni East 110,376
- Kieni West 88,525
- Mathira East 99,065
- Mathira West 59,895
- Nyeri South 91,081
- Mukurwe-ini 89,137
- Nyeri Central 140,338
- Mt. Kenya Forest 188
- Aberdare Forest 106
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
- ↑ A REVIEW OF NYERI COUNTY-KENYA STRATEGIC PLAN 2013 – 2017, iliwekwa mnamo 29/04/2018
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-04.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
![]() | Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kaunti ya Nyeri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |