Kitale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kitale
Kitale is located in Kenya
Kitale
Kitale
Mahali pa mji wa Kitale katika Kenya
Majiranukta: 1°01′0″N 35°0′0″E / 1.01667°N 35°E / 1.01667; 35
Nchi Kenya
Mkoa Bonde la Ufa
Wilaya Trans-Nzoia
Idadi ya wakazi
 - 63,254

Kitale ni mji wa Kenya katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Ni makao makuu ya kaunti ya Trans-Nzoia.

Mji upo mita 1900 juu ya usawa wa bahari. Hifadhi ya taifa ya Saiwa Swamp iko karibu na mji, ambao unajulikana pia kwa makumbusho ya Kitale [1].

Mazao ya sokoni inayokuzwa katika sehemu hii ni majani ya chai, kahawa, pareto, alizeti, maharagwe na mahindi. Kitale ni soko la mazao ya kilimo na kituo cha kilimo cha mseto.

Mji huu ulianzishwa mwaka wa 1908 na Wazungu walowezi. Reli ya Uganda kutoka Eldoret ilifika Kitale mwaka wa 1926 na ilichangia kukuza mji huu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Anwani ya kijiografia: 1°01′N 35°00′E / 1.017°N 35°E / 1.017; 35