Kaunti ya Makueni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kaunti ya Makueni
Kaunti
Haven of Opportunities
Makueni County in Kenya.svgMakueni County in Kenya.svg
Kaunti ya Makueni katika Kenya
Nchi Flag of Kenya.svg Kenya
Namba 17
Ilianzishwa Tarehe 4 Machi, 2013
Ilitanguliwa na Mkoa wa Mashariki
Makao Makuu Wote
Miji mingine Emali, Makindu, Kibwezi, Mtito Andei
Gavana Prof. Kivutha Kibwana, EGH
Naibu wa Gavana Adelina Mwau Ndeto, OGW
Seneta Mutula Kilonzo Junior
Mbunge Mwanamke(Bunge la Taifa) Rose Mumo
Bunge la Kaunti Bunge la Kaunti ya Makueni
Wawakilishi wa Bunge la Kaunti waliochaguliwa 30
Maeneo bunge/Kaunti ndogo 6
Eneo 8,008.9 km2 (3,092.3 sq mi)
Idadi ya watu 884,527
Kanda muda Saa za Afrika Mashariki (UTC+3)
Tovuti makueni.go.ke

Kaunti ya Makueni ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Makao makuu yako Wote.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Makueni imepakana na Machakos (kaskazini), Kitui (mashariki), Taita Taveta (kusini) na Kajiado (magaribi). Ni kaunti nusu kavu. Tabianchi hii huiwezesha Makueni kuzalisha maembe kwa muda mrefu kwa mwaka.

Mto Athi hupitia katika mpaka wa mashariki. Kulingana na utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, asilimia 39 ya Makueni ina maji chini ya ardhi[1].

Tambarare ya Yatta huwa katika kaskazini mwa kaunti. Vilima vya Chyulu na Mbuga ya Kitaifa ya Vilima vya Chyulu huwa kusini mwa kaunti.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Makueni imegawanywa katika maeneo yafuatayo:

Eneo bunge Wadi
Mbooni Tulimani, Mbooni, Kithungo/Kitundu, Kiteta/Kisau, Waia-Kako, Kalawa
Kilome Kasikeu, Mukaa, Kiima Kiu/Kalanzoni
Kaiti Ukia, Kee, Kilungu, Ilima
Makueni Wote, Muvau/Kikuumini, Mavindini, Kitise/Kithuki, Kathonzweni,  Nzau/Kilili/Kalamba, Mbitini
Kibwezi West Makindu, Nguumo, Kikumbulyu North, Kimumbulyu South, Nguu/Masumba, Emali/Mulala,
Kibwezi East Masongaleni, Mtito Andei, Thange, Ivingoni/Nzambani

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Hope in Tapping Underground Water in Makueni - Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology. Iliwekwa mnamo 2018-04-26.