Nyahururu
Mandhari
Nyahururu | |
Mahali pa mji wa Nyahururu katika Kenya |
|
Majiranukta: 0°2′0″N 36°22′0″E / 0.03333°N 36.36667°E | |
Nchi | Kenya |
---|---|
Kaunti | Laikipia |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 51,434 |
Nyahururu ni mji wa Kenya katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Mji uko Mashariki kwa Nakuru kwenye mita 2,303 juu ya UB.
Ni sehemu ya kusini magharibi ya Kaunti ya Laikipia.
Mji huu ulianzishwa kwa jina la Thomson Falls kutokana na maporomoko ya mto Ewaso Narok unaotiririka kutoka milima ya Aberdare.
Mji huu ulimea pamoja na kituo cha reli iliyoishikanisha na mji wa Gilgil. Nyahururu ilikuwa penye viwanda vya National Pencil, ambayo ilifungwa, na Kenya Cooperative Creameries. Chuo kikuu cha Egerton lina shule huko Nyahururu na kuna shule kadhaa za binafsi.
Mwaka 2009 ulikuwa na wakazi 51,434[1].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Sensa ya Kenya 2009 Ilihifadhiwa 9 Januari 2019 kwenye Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Nyahururu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |