Kajiado

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Kajiado
Kajiado is located in Kenya
Kajiado
Kajiado
Mahali pa mji wa Kajiado katika Kenya
Viwianishi: 1°51′0″S 36°47′0″E / 1.85°S 36.78333°E / -1.85; 36.78333
Nchi Kenya
Mkoa Bonde la Ufa
Wilaya Kajiado
Idadi ya wakazi
 - 8,128

Kajiado ni mji wa Kenya katika Mkoa wa Bonde la Ufa. Mji huu upo kusini mwa mji wa Nairobi katika barabara kuu ya Nairobi- Arusha. Idadi ya watu wanaoishi Kajiado ni 8198 (sensa ya 1999) [1]. Idadi kubwa ya watu wanaoishi kajiado ni wa asili ya kimaasai.

Mji wa Kajiado ni mji mkuu wa Wilaya ya Kajiado.

Jina la Kajiado linatokana na neno "Orkejuado" ambalo linamaanisha "mto mrefu" katika lugha ya kimasai. Mto huu upo magharibi mwa mji huu.

Jina halisi wa mjii huu ni "Olopurupurana", ambalo linamaana "kilima cha mviringo".

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Kajiado una kituo katika barabara ya reli ya Magadi Soda Railway ambaye inatokea Konza mpaka Magadi.Pia kuna vituo vya matatu za kwenda Namanga na Nairobi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]