Kaunti ya Laikipia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Kaunti ya Laikipia, Kenya

Kaunti ya Laikipia ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 518,560 katika eneo la km2 9,532.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 54 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yanatarajiwa kuwa Rumuruti,lakini yamesalia kuwa Nanyuki.

Kaunti hii ina vituo viwili vikuu vya soko: Nanyuki upande wa kusini mashariki, na Nyahururu upande wa kusini magharibi.

Wakikuyu ni takribani 60% ya idadi ya watu wote kwenye kaunti hiyo, huku idadi iliyosalia ikijumuisha watu wa makabila mengine, ni pamoja na Wamasai, Wasamburu, Wameru, Waborana, Wakalenjin, Wasomali, Waturkana, Wazungu na watu wa asili ya Asia. Mashamba mengi yanamilikiwa na idadi ndogo ya walowezi.

Shughuli kuu za kiuchumi ni utalii na kilimo, hasa mimea ya nafaka, ufugaji na kilimo cha maua, matunda na mboga. Uhaba wa maji ni kero kubwa na chanzo cha visa vingi vya kiusalama baina ya wafugaji wa kuhamahama na wenye mashamba.

Hali ya hewa ni ya baridi kiasi, ikiwa na msimu wa mvua na kiangazi.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Nandi ina maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eneo bunge Kata
Laikipia Kaskazini Sosian, Segera, Mugogodo West, Mugogodo East
Laikipia Mashariki Ngobit, Tigithi, Thingithu, Nanyuki, Umande
Laikipia Magharibi Ol-Moran, Rumuruti, Township, Githiga, Marmanet, Igwamiti Salama

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3][hariri | hariri chanzo]

  • Laikipia Central 95,594
  • Laikipia East 102,815
  • Laikipia North 36,184
  • Laikipia West 129,263
  • Nyahururu 154,704

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. http://countytrak.infotrakresearch.com/Laikipia-county/
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.