Nenda kwa yaliyomo

Vihiga

Majiranukta: 0°3′0″N 34°43′30″E / 0.05000°N 34.72500°E / 0.05000; 34.72500
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vihiga ni mji wa Kenya magharibi ulioko upande wa mashariki wa Msitu Kakamega. Mji huu uko kando ya barabara ya Kisumu na Kakamega na kilomita tano tu kaskazini kwa ikweta.

Vihiga imetoa jina lake kwa kaunti ya Vihiga ambayo makao makuu yake yako Mbale iliyoko katika manispaa ya Vihiga. Manispaa hiyo ina wakazi 118,696 (sensa ya mwaka 2009[1]).

Manispaa ya Vihiga ina wadi sita, mbili kati ya hizo (Central Maragoli na Wamuluma) ziko katika eneo bunge la Vihiga huku nne zilizobaki (Chavakali, Izawa, Lyaduywa na Maragoli Kaskazini) ni sehemu ya eneo bunge la Sabatia. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2002, viti vyote sita vya baraza vililishindwa na National Rainbow Coalition.

Wamaragoli ndio kabila kuu katika eneo hili na mji huu hujulikana pia wakati mwingine kama Maragoli. Watu wanaoishi Vihiga hujitambulisha kimsingi kama "Wamaragoli" na wanazungumza lugha inayoitwa Kimaragoli. Lugha hiyo ni tofauti kabisa kati ya makabila mengine ya Waluhya na ndiyo lugha ya kwanza ya Kiluhya kutumika kutafsiria Biblia. Wengi wa Wamaragoli waliongokea Ukristo ndani ya madhehebu ya ya Quaker, ambayo bado inafuatilia hadi leo. Watiriki, Waidakho na Wabanyore ndio makabila mengine katika eneo hili.

Vihiga pia ni jina la moja ya divisheni ndani yake. Divisheni nyingine ni pamoja na Sabatia, Hamisi, Lwanda na Emuhaya.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sensa ya Kenya 2009 Archived 9 Januari 2019 at the Wayback Machine., tovuti ya KNBS, ilitazamwa Januari 2009.

0°3′0″N 34°43′30″E / 0.05000°N 34.72500°E / 0.05000; 34.72500