Nenda kwa yaliyomo

Kaunti ya Narok

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya ramani ikionesha eneo la Kaunti ya Narok, Kenya
Barabara ya Keekorok ya kuelekea Narok

Kaunti ya Narok ni mojawapo ya kaunti 47 za Kenya, iliyoko katika eneo la kusini magharibi mwa nchi katika Mkoa wa zamani wa Bonde la Ufa. Inapakana na Kaunti ya Bomet na Kaunti ya Nakuru upande wa mashariki, Kaunti ya Migori na Kaunti ya Kisii upande wa magharibi, na Tanzania upande wa kusini. Kaunti hii ina idadi ya watu takriban 1,157,873 kulingana na sensa ya mwaka 2019 katika eneo la km2 17,950.3, msongamano ukiwa hivyo wa watu 65 kwa kilometa mraba[1], na ni mojawapo ya maeneo makuu ya makazi ya jamii ya Wamaasai. Mji wa Narok ndio makao makuu ya kaunti na pia kituo kikuu cha kibiashara. Narok inajulikana kwa utalii hasa kupitia Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara, kilimo cha ngano na ufugaji wa mifugo kama vile ng’ombe na kondoo, pamoja na utamaduni tajiri wa jamii ya Wamaasai.

Kaunti ya Narok imegawanywa katika maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eneo bunge Kata
Emurua Dikirr Ilkerin, Ololmasani, Mogondo, Kapsasian
Kilgoris Kilgoris ya Kati, Keyian, Angata Barikoi, Shankoe, Kimintet, Lolgorian
Narok Magharibi Ilmotok, Mara, Siana, Naikarra
Narok Mashariki Mosiro, Ildamat, Keekonyokie, Suswa
Narok Kaskazini Olpusimoro, Olokurto, Narok Mjini, Nkareta'Olorropil, Melili
Narok Kusini Majimoto/Naroos, Ulolulung'a, Melelo, Loita, Sogoo, Sagamian

Demografia

[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3]

[hariri | hariri chanzo]
  • Narok East 115,323
  • Narok North 251,862
  • Narok South 238,472
  • Narok West 195,287
  • Trans Mara East 111,183
  • Trans Mara West 245,714
    • Mau Forest 32

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-09-01. Iliwekwa mnamo 2021-09-01.
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.