Wilaya ya Trans Mara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wilaya ya Trans Mara ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Bonde la Ufa wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010). Iliundwa mwaka wa 1994 kutokana na Wilaya ya Narok.

Makao makuu yalikuwa mjini Kilgoris.

Kwa sasa imekuwa tena sehemu ya kaunti ya Narok.

Wilaya hii ilikuwa na jumla ya wakazi 170,591 (sensa ya 1999) na ukubwa wa eneo wa kilomita mraba 2,846 [1].

Mara Triangle (ambayo ni sehemu ya hifadhi ya Masai Mara) ilikuwa katika wilaya ya Trans-Mara.

Wilaya hii ilikuwa na serikali moja tu ya mtaa, Baraza la Mji wa Trans Mara.

Eneo Bunge la Kilgoris ndilo eneo bunge la pekee katika wilaya hii hadi leo.

Maeneo ya utawala
Tarafa Idadi ya Watu* Wakaazi wa mjini* Makao makuu
Keiyan 25,885 1,277 Enoosaen
Kilgoris 31,827 4,497 Kilgoris
Kirindoni 56,197 0
Lolgorian 25,553 1,410 Lolgorien
Pirrar 31,129 0
Jumla 170,591 7,184 -
* Sensa ya 1999 census|. Sources:[2][3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]