Wilaya ya Gucha
Wilaya ya Gucha (pia: Wilaya ya Kisii Kusini au Wilaya ya Ogembo) ilikuwa wilaya mojawapo ya Mkoa wa Nyanza wa Jamhuri ya Kenya hadi ilipopitishwa katiba mpya ya nchi (2010).
Makao makuu yalikuwa Ogembo, yenye wakazi zaidi ya elfu moja na zaidi ya watu elfu moja ambao huitembelea kila siku.
Kwa sasa imekuwa sehemu ya kaunti ya Kisii.
Wakazi wake walikuwa takriban 461,000 (1999) [1] Archived Mei 21, 2005 at the Wayback Machine.. Idadi kubwa ya watu ni Wakisii, lakini hupakana na ardhi ya masai huko kusini-mashariki. Kumekuwa na mapigano kadhaa ya kikabila baina yao.
Kilimo ndiyo sekta kuu. Mbali ya mashamba mengi madogo madogo, kuna mashamba makubwa ya miwa.
Wilaya hii ilikuwa na majimbo matatu: South Mugirango, Bomachoge na Bobasi. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2002 viti vyote vitatu vilishindwa na chama cha Ford-People.
Mamlaka za Mitaa (Halmashauri) | |||
Mamlaka | Aina | Idadi ya Watu | Wakazi wa mjini* |
---|---|---|---|
Ogembo | Jiji | 48.725 | 1.654 |
Nyamarambe | Jiji | 40.232 | 212 |
Nyamache | Jiji | 38.924 | 2.205 |
Tabaka | Jiji | 26.325 | 5.067 |
Gucha | County | 306.733 | 1.946 |
Jumla | -- | 460.939 | 11.084 |
* 1999 census. Source: [2] |
Maeneo ya utawala | |||
Tarafa | Idadi ya Watu | Wakazi wa mjini* | Makao makuu |
---|---|---|---|
Etago | 59.652 | 0 | |
Kenyenya | 92.641 | 1.857 | |
Nyacheki | 56.998 | 405 | |
Nyamache | 54.722 | 1.702 | |
Nyamarambe | 67.060 | 3.850 | |
Ogembo | 78.827 | 1.465 | Ogembo |
Sameta | 51.039 | 0 | |
Jumla | 460.939 | 9.279 | -- |
* 1999 census. Sources: [3], [4], |
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Lugha
- [http://web.archive.org/20070510231620/http://www.ekegusii.org/ Archived Mei 10, 2007 at the Wayback Machine. Lugha ya Kisii - Kisii / Tafsiri ya Kiingereza-Ekegusii
![]() | Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Gucha kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |