Wakisii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kisii (hujulikana pia kama Gusii) ni jamii ya Kibantu ambao hukaa katikaWilaya ya Kisii katika Mkoa wa Nyanza, Magharibi mwa Kenya.

Mji wa Kisii - unaojulikana kama Bosongo kwa wakazi wake - uko katika Mkoa wa Nyanza, kusini magharibi mwa Kenya na ni nyumbani kwa watu wa asili ya Gusii. Jina Bosongo liliaminiwa kutokana na jina Abasongo (kwa maana ya Wazungu) ambao waliishi katika mji wakati wa ukoloni. Kulingana na sensa ya mwaka 1979, Wilaya ya Kisii ilikuwa na wakazi 588.000.

Asili ya Abagusii[hariri | hariri chanzo]

Waabagusii pamoja na makundi mengine ya kibantu wanaaminika kuwa na asili ya Kongo (inayojulikana sasa kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo). Kuhama kwao kunaaminika kuwa kulitokana na wakazi zaidi, uhaba wa chakula, migogoro kati yao na udongo uliopoteza uzuri wake kwa ajili ya kilimo. Wabantu walipokuwa wakitoka Kongo, wao waligawanyika katika makundi mbalimbali na wakisii waliishia kuishi katika Mkoa wa Nyanza karibu na Ziwa Victoria.

Wakisii waliishia katika eneo la kijiografia ya kipekee miongoni mwa makundi ya kibantu kwani walikuwa wamezungukwa pande zote na makundi ya kiuadui yakinailoti ya Wajaluo, Kipsigis, Nandi, na Wamaasai. Ubishani usioisha uliwafanya wawe na desturi ya vita ili wajipinge dhidi ya wezi wa mifugo. Hadi siku hii, wana sifa ya kuwa wagumu, wasiopoteza roho haraka, na wanaofanya kazi sana.

Wakisii Leo[hariri | hariri chanzo]

Wakisi wanajulikana kama mojawapo ya jamii zinazojishughulisha zaidi kenya, waliobarikiwa na mashamba makubwa ya chai, kahawa na mashamba ya ndizi. Hata hivyo, wilaya ya Kisii ina msongamano mkubwa sana wa watu. Ni moja ya maeneo yaliyo na watu wengi sana nchini Kenya (baada ya miji ya Nairobi na Mombasa), na yenye watu wengi zaidi katika maeneo ya mashambani. Pia ina moja ya idadi kubwa zaidi ya uzalishaji nchini kenya(kama inavyothibitishwa na mfululizo wa demographia na utafiti). Idadi ya uzalizashi katika jamii ya makisii ni mojawapo ya za juu zaidi ulimwenguni, (angalia Kenya Conundrum: A Regional Analysis of Population Growth and Primary Education (Paperback) by Juha I. Uitto [Mwandishi]). Mambo haya yamefanya wakisii kuwa miongoni mwa jamii zilizoenea zaidi kijiografia katika Afrika Mashariki. Idadi kubwa ya wakisii pia imeenda ugenini kutafuta masomo ma maisha mazuri zaidi. Wakisii ni baadhi ya Wakenya wengi zaidi kuwakilishwa katika vyuo vikuu vya kigeni (kawaida India na Marekani). Majina kama Mogeni, Bogonko, Osebe, Bosire, Moseti, Onkoba, Onchiri, Isaboke, Kiberi, mogaka na wengine ni majina ya familia ya kawaida tu kama Smith na Johnson katika tamaduni za Anglo-Saxon. Majina ya kike kama Moraa, Nyanchama, Nyaboke, Kemunto, Kwamboka, Kerebi na mengine pia ya kawaida yaliyopewa wasichana.

Kilimo Kisii[hariri | hariri chanzo]

Kitambo, Kisii ilikuwa na misitu mikubwa, pamoja na miti iliyozeekana yenye matawi pana. Ilikuwa ni sehemu ya msitu wa Bonde la Kongo. Mabaki ya pekee ya msitu huu Kenya ni msitu Kakamega, ambao ni pembe magharibi zaidi ya msitu wa Equator.Maeneo mawili ya misitu huo yalikuwa yanaunganishwa kupitia Nandi na Kericho, kabla ya maeneo ya Nandi na Kericho kukatwa miti ili chai ipandwe na matu wakae pale.

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Wao wanazungumza lugha ya Kisii au kama inavyojulikana Ekegusii miongoni mwa wasemaji. Hata hivyo, baadhi ya makala ya kitambo huita jamii hii Kosova. Lugha hii na lugha nyingine za Kibantu ni sawa sana. Wameru katika jimbo la Mashariki wanafanana sana na wakisii katika lugha na utamaduni.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Wakisii hucheza kiungo kikubwa cha muziki kiitwacho obokano. Kutahirishwa kwa vijana wenye umri wa miaka 10 bila dawa za kupunguza uchungu. Tohara ni moja wapo ya sherehe ambapo vijana walijifunza jinsi ya kuishi na kuheshimu wakuu wao. Vijana ambayo walikuwa wanatahiriwa walifunzwa jinsi ya kijitahidi katika kutafutia jamii yao.

Orodha ya baadhi ya Wakisii mashuhuri[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]