Wanandi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Askari watatu wa Kinandi.

Wanandi ni jina la kabila dogo la Waniloti ambalo huhesabiwa katika kabila kuu la Wakalenjin.

Wanakadiriwa kuwa 949,000[1] na kuishi hasa katika kaunti ya Nandi nchini Kenya.

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Wao huongea Kinandi, lahaja ya lugha ya Kikalenjin, mojawapo ya lugha za Kiniloti.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ujenzi wa reli kutoka Mombasa kwenye bahari ya Hindi hadi Kisumu kwenye ziwa Viktoria ulianza mwaka wa 1895 na ulimalizika mwaka wa 1901. Ujenzi huo uliwezesha wakoloni kutoka Uingereza kuingia ndani kabisa mwa Kenya. Hii ilikuwa sehemu ya kwanza ya reli ya Uganda.

Katika ujenzi wa reli, Waingereza walikumbana na upinzani mgumu, hasa kutoka kwa Koitalel Arap Samoei, kiongozi wa Kinandi na mwaguzi aliyetabiri ya kwamba nyoka mweusi atapita katikati ya eneo la Nandi akitema mate ya moto. Nyoka alikuwa anaashiria reli. Kwa miaka kumi Samoei alipigana dhidi ya wajenzi wa reli na gari la moshi. Baadaye, Samoei aliuawa na Waingereza kwani walikuwa na dhamira ya kuendelea na kumaliza reli hii.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. www.ethnologue.com

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wanandi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.