Wachonyi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wachonyi ni mojawapo kati ya makabila tisa ya pwani ya Kenya.

Hupatikana katika maeneo ya Mtwapa,hadi kupakana na Wagiryama upande wa Kaloleni na Kilifi na pia Wamepakana na Wakauma upande wa Mavueni, na Jaribuni

Wachonyi huwa na mbari au koo kwa mfano:

 1. Wamwakomola
 2. Wamwarumba
 3. Waborani
 4. Wamwakiti
 5. Wamwachapkwe
 6. Wamwagambo
 7. Wabuta
 8. Wadzakaa
 9. Wamongwe
 10. Wamwari
 11. Waremere

Wachonyi ni watu ambao huishi kwa pamoja kama familia na pia hukubali wanaume kuoa bibi zaidi ya mmoja. Pia hufanya kitendo cha "kuingiliana ufa", kumaanisha kwamba mtu huweza kuoa bibi ya ndugu yake iwapo amekufa; hivyo basi kumrithi bibi ya nduguye.

Wachonyi hujulikana kama wafanyabiashara wa pwani kwani hupatikana takriban kila pahali pwani wakifanya biashara.

Pia hujihusisha na kilimo cha kujikimu wao wenyewe na pia kwa kuuza.

Wachonyi idadi kubwa yao ni Wakristo, japo kuna asilimia chache sana Waislamu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wachonyi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.