Wakamba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kazi ya Kikamba katika duka la Mombasa

Wakamba ni kabila kubwa nchini Kenya wakikalia eneo la Ukambani kati ya Nairobi, Voi na kati ya mlima Kenya na mlima Kilimanjaro.

Asili yao inaaminika kuwa katika eneo la Kilimanjaro mwenyewe lakini walihama takriban miaka 400-500 iliyopita kuja Ukambani walipo.

Hutumia lugha ya Kikamba ambacho ni lugha ya Kibantu karibu na Kigikuyu, Kiembu na Kimeru.

Wakamba ni kabila kubwa la nne nchini Kenya.

Maisha kabla ya ukoloni[hariri | hariri chanzo]

Walikuwa wafugaji, wakulima na wavindaji. Katika karne ya 19 walikuwa na nafasi muhimu katika biashara ya pembe ya ndovu kati ya bara na pwani la Kenya. Misafara yote kutoka au kwenda Mombasa ilipaswa kupita katika eneo lao. Walitafutwa sana kama wapagazi.

Maisha wakati wa ukoloni[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia miaka ya 1930 Wakamba walianza kujiunga kwa wengi na jeshi na polisi ya kikoloni. Imekadiriwa kuwa karibu theluthi moja ya Wakamba wote walioajiriwa walikuwa jeshini. Mwendo huu ulisababishwa na ugumu wa maisha kutokana na ukame wa Ukambani kwa upande moja na hali ya kukaa karibu na reli na taasisi za dola la kikoloni.

Wakati wa vita ya Mau Mau sehemu za Wakamba walijiunga na harakati ile lakini wanajeshi kwa ujumla walisimama upande wa serikali ya kikoloni.

Katika kilimo Wakamba walianza kilimo cha umwagiliaji.

Sanaa[hariri | hariri chanzo]

Wasanii Wakamba wamekuwa maarufu kama wachongaji wa ubao nchini Kenya. Katika historia yao hutunza kumbukumbu ya kwamba wakati wa ukoloni Mkamba alifika Dar es Salaam alipojifunza sanaa hii kutoka wachongaji Wamakonde na kurudi na maarifa alipofundisha wengine. Leo hii ni hasa Wakamba wanaochonga sanamu za wanyama wa pori zinazotafutwa na kununuliwa na watalii.

Wakamba maarufu[hariri | hariri chanzo]

  • Mutava Musyimi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Kenya
  • Kalonzo Musyoka aliyekuwa waziri katika serikali mbalimbali na mgombea wa urais 2008
  • Charity Ngilu aliyekuwa mgombea wa urais 1997 na waziri katika serikali ya Rainbow 2002-2007.
  • John S. Mbiti mtaalamu wa dini za Afrika
  • David Maillu mwandidhi wa riwaya za Kiswahili na Kiingereza

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]