Mau mau

Mau mau lilikuwa kundi la wapiganaji wa Kenya waliokuwa wakipinga utawala wa kikoloni wa Waingereza toka mwaka 1952 hadi 1960. Harakati zao (kwa Kiingereza: Maumau uprising, Maumau rebellion) ziliongozwa na Wakikuyu na zilijitokeza kutokana na kutoridhika kwa wingi wa watu kuhusu kupokonywa ardhi, ukandamizaji wa kisiasa, na kukosa usawa wa kijamii. Vikatokea vita vya kishujaa na matendo ya uharibifu dhidi ya serikali ya kikoloni na wakoloni wenyewe.
Waingereza walijibu kwa mbinu kali za kijeshi, zikiwa ni pamoja na kazi ya lazima, mateso ya watu wengi, na mauaji.
Urithi wa uasi huu bado ni kipengele muhimu katika historia ya Kenya, ikiashiria upinzani dhidi ya ukoloni na mapambano ya kudai haki. [1]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Kundi lilianzishwa mwaka wa 1946, na viongozi wa hao mashujaa walikuwa Jomo Kenyatta, Jaramogi Oginga Odinga, Paul Ngei, Ronald Ngala, Harry Thuku na wengineo.
Walifanya kazi nzuri sana, kwanza juu ya kuonyesha vile watu wanavyoweza kufika mbali wakiwa kitu kimoja. Kama haingekuwa kwa maungano hawangeweza kufanya chochote.
Ingawa vuguvugu la Mau mau halikuwa na mafanikio makubwa kijeshi, upinzani wao ulichangia sana katika kuharakisha upatikanaji wa uhuru wa Kenya mwaka 1963.
Jina
[hariri | hariri chanzo]Chanzo cha jina la kundi hili, Mau mau, hakieleweki vyema. Kuna hali ya kutokukubaliana juu ya chanzo na maana ya jina lenyewe. Baadhi wanadai kuwa ni jina la vilima fulani huko Kenya, wengine wanaamini kuwa jina hilo lilitoka kwa walowezi wa Kiingereza lililokuwa na nia ya kudhalilisha kundi hilo. Wako pia wanaosema kuwa jina hilo ni kifupi cha: "Mzungu Aende Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru".
Sehemu kubwa ya kundi la Mau mau iliundwa na watu wa kabila la Gikuyu huku kukiwa na baadhi ya wanachama toka Embu na Meru. Wagikuyu wenyewe hawakuwa wakiliita kundi hili Mau mau bali "Muingi" (vuguvugu), "Muigwithania" (anayeunganisha), "Muma wa Uiguano" (kiapo cha umoja) au KCA (Kenya Central Association, chama kilichotangulia kupigania haki za Wakikuyu.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mau mau kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |