Charity Ngilu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Charity Ngilu

Charity Kaluki Ngilu (* 1952) ni mwanasiasa Mkenya aliyekuwa waziri wa afya katika serikali ya rais Mwai Kibaki kuanzia 2002 hadi 2007.

Ngilu alizaliwa katika Ukambani wilaya ya Makueni mwaka 1952. Alifanya kazi na Benki Kuu ya Kenya hadi kuanzisha kampuni yake ya vifaa vya plastiki. Aliolewa na Michael Mwendwa Ngilu aliyeaga dunia mwaka 2006. Amezaa watoto watatu.

Aliingia katika siasa ya upinzani mwaka 1991 aligombea na kushindi kiti cha mbunge wa Kitui Kati kwa chama cha Democratic Party (DP) cha Mwai KIbaki.

1997 aliondoka katika DP akiandaa kugombea urais yeye mwenyewe akiwa mwanamke wa kwanza nchini wa kugombea urais. Akajiunga na chama cha SDP akamaliza nafasi ya tano.[1]

Baadaye akajiunga na National Party of Kenya akashiriki katika maungano ya upinzani ya NAK kwa uchaguzi wa 2002. NAK iliunga mkono na LDP ya Raila Odinga kuwa NARC.

Ngilu alikuwa mwenyekiti wa chama kipya cha National Alliance of Rainbow NARC akajipatia jina la "Mama Rainbow".

Katika serikali ya KIbaki alikuwa waziri wa afya.

Oktoba 2007 alitangaza kusimama upnade wa ODM akaachishwa katika serikali.

Alirudishwa bungeni mwaka 2007 kwa tiketi ya NARC.

  1. Special Report Kenya: candidates and issues (BBC 1997)