Nenda kwa yaliyomo

Wamijikenda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mijikenda)

Mijikenda ("miji au makabila tisa": "kenda" ni Kiswahili asilia kwa namba 9) ni jina la kutaja jumla vikundi tisa kwenye pwani ya Kenya. Vikundi hivi wakati mwingine huitwa koo, wakati mwingine makabila. Watazamwa kuwa vikundi ya pekee vinavyoshiriki lugha moja kwa lahaja mbalimbali.

Idadi yao ilikuwa takriban 750,000 mnamo mwaka 1980.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Utamaduni wa Mijikenda ulikua na kuendelea katika mazingira ya miji ya Waswahili lakini tofauti na Waswahili wenyewe. Kwa jumla waliwahi kuitwa na watu wa nje pia "Wanyika" yaani watu wa porini.

Katika kumbukumbu yao wenyewe asili yao ilikuwa eneo la Singwaya au Shungwaya kaskazini mwa Somalia wakasukumwa kwenda kusini na uenezi wa Waoromo.

Wataalamu wengine hukubali kiini cha kweli katika masimulizi hayo, wengine huona mijikenda ni kundi lililotokana na vikundi mbalimbali.

"Mji" wa jina "Mijikenda" ulikuwa kiasili mahala pa kaya au mahali patakatifu ambako kundi likakusanyika kupeleka maombi kwa mizimu. Kaya hizo zatunzwa hadi leo, hata kama idadi kubwa wamekuwa ama Waislamu au Wakristo. Ziko kwenye vilima vilivyopo nyuma ya pwani yenyewe.

Vikundi hivi tisa ni:

Wadigo wako kusini kabisa, wakiingia hadi Tanzania ya leo.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Lua error in package.lua at line 80: module 'Module:Navbar/configuration' not found.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamijikenda kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.