Kenda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mabadiliko katika kuandika tisa.

Kenda ni Kiswahili asilia kwa namba 9. Kwa kawaida inaandikwa 9 lakini IX kwa namba za Kiroma na ٩ kwa zile za Kiarabu.

Neno hili ni la asili ya Kibantu. Siku hizi neno "tisa" ambalo ni neno leye asili ya Kiarabu hutumiwa zaidi kutaja namba 9, pamoja na tisini (tisa mara kumi).

Kamusi za mwanzo na katikati ya karne ya 20 kama M-J SSE zinasema ya kwamba "kenda" iliwahi kutumiwa sawa na "tisa".

Siku hizi matumizi yake imepungua sana.

Mfano wa matumizi yake ni katika jina Mijikenda linalotaja kundi la makabila au koo 9 za Kenya.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]