Standard Swahili-English Dictionary

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka M-J SSE)

Madan-Johnson's Standard Swahili-English Dictionary (kifupi: M-J SSE) iliandaliwa na wataalamu wa "Inter-territorial Language (Swahili) committee to the East African Dependencies" baada ya Vita Kuu ya Kwanza kwa ajili ya maeneo chini ya utawala wa Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Kamati hiyo iliandaa kamusi mbili za Kiingereza-Kiswahili (M-J SES) na pia Kiswahili-Kiingereza.

Mhariri Mkuu wa kamati alikuwa katibu yake Frederick Johnson. Msingi wa kamusi hizi ulikuwa kazi ya A. C. Madan. Hivyo kamusi hizo hutajwa kama "Madan-Johnson".

Mara nyingi lugha ya kamusi hizi si tena Kiswahili cha kisasa. Lakini zimeendelea kuchapishwa mara nyingi hadi wakati wa kisasa.

Sifa ya kamusi hii ni maelezo mazuri kuhusu asili ya maneno, hasa ya maneno yenye asili katika lugha za Kiarabu, Kiajemi na lugha mbalimbali za Kibantu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Madan-Johnson, A Standard Swahili-English Dictionary (hutolewa na Oxford University Press, Nairobi & Dar es Salaam, 1939 na kuchapishwa upya mara nyingi)
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Standard Swahili-English Dictionary kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.