Wakalenjin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Pokot-Frauen.

Wakalenjin ni kundi la makabila ya magharibi mwa Kenya, hasa katika uliokuwa mkoa wa Bonde la Ufa, wanaoongea lugha za Kiniloti zilizo karibu. Wasemaji wa lugha hizo wako pia Tanzania na Uganda.

Kati ya vikundi hivi ni Waelgeyo, Wakipsigis, Wamarakwet, Wanandi, Wasabaot, Waterik na Watugen. Mababu wao walihamia Kenya kutoka Sudani karne nyingi zilizopita na wengine wanakadiria wamefika tayari tangu miaka 2,000.

Wakati mwingine hata Wapokot wanahesabiwa kati ya Wakalenjin lakini kwa kawaida wanajitazama kama kundi la pekee hata kama lugha yao ni ya karibu.

Utamaduni wao unaonyesha dalili za mapokeo ya wafugaji lakini walio wengi ni wakulima.

Katika karne ya 20 makabila hayo yalianza kujenga umoja wao na kujielewa kama jumuiya moja. Waingereza waliwaita "makabila wenaosema Kinandi". Neno 'Kalenjin' linamaanisha "nakuambia" kwa lugha ya Kinandi: lilikuwa jina la programu ya redio iliyosikilizwa na watu wengi katika bonde la Ufa na kuwa jina la pamoja.

Leo takriban asilimia 12 za Wakenya huhesabiwa kati ya Wakalenjin.

Wakalenjin wamepata umaarufu kwa sababu wanamichezo wengi Wakenya waliofaulu kimataifa, hasa wakimbiaji, ni Wakalenjin, kama vile Paul Tergat na wengine wengi.

Rais wa pili wa Kenya Daniel Arap Moi alikuwa Mkalenjin.

Mfano wa lugha: Sala ya Baba Yetu kwa Kikalenjin[hariri | hariri chanzo]

Kwandanyo ne mi barak kipsengwet,
Ingotililit kaineng'ung.
Ingonyo bounateng'ung.
Ingoyaak eng' ng'ony mageng'ung',
Ko u ye kiyaei eng' kipsengwet.
Konech rani amitwogikyok che bo ra.
Ak inyoiywech kaat lelutikyok,
ko u ye kinyochini kaat che lelwech.
Amemutech ole mi yomset,
ago soruech eng' ne ya.
Amu neng'ung' bounatet, ak kamuktaet, ak torornatet, agoi koigeny.
Amen.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Flag of Kenya.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakalenjin kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.