Wamarakwet

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Marakwet pia ni wilaya nchini Kenya, tazama pia Wilaya ya Marakwet

Marakwet ni jina lililobadilishwa kutoka Markweta. Ni kabila ndogo katika babila kuu la Kalenjin idadi yao ikikadiriwa kuwa 200 000. Inajumuisha kabila ndogo za Almoo, Cherangany (Sengwer au Kimaala), Endoow, Markweta (kabila ndogo inalolipa jina lake la kawaida) Sombirir (Borokot) na Kiptaani ambao ndio wanaishi kwa wingi katika Wilaya ya Marakwet eneo la Kaskazini ya Bonde la Ufa nchini Kenya. Wengine wao wanaishi katika wilaya za Trans Nzoia Mahariki na Uasin Gishu Kaskazini na miji mingine nchini Kenya. Wachache wameenda kuishi katika maeneo ya mbali kama vile Australia, Southern Africa, na hata Tennessee/Washington / New York nchini Marekani. Baadhi ya wakimbiaji wa masafa marefu wakuu na haswa wa kuruka viunzi duniani wametoka hutoka miongoni mwa kabila hili.


Wao huishi maisha yanaojumuisha ukulima wa kujikimu pamoja na ufugaji wa ng'ombe za gredi,kondoo na kuku. Wao hupanda sanasana mahindi, viazi, maharagwe na mboga katika maeneo ya milima. Wale wanaoishi katika sehemu ya vilima na katika Kerio Valley hukuza sana mbuzi na ng'ombe wa nyama ya zebu na hupanda mtama, wimbi, mihogo, mboga na matunda haswa maembe na machungwa. Kuna mfumo usioeleweka wa kale sana wa kunyunyiza maji wa mitaro ambao hukimi mimea hizi kando ya Bonde la Kerio ambao unaaminika kuweko kwa zaidi ya miaka 500.


Wamarakwet walijitenga katika vikundi/sehemu/makabila ambao hawakutambua mamlaka zaidi kuliko asiswo (mkusanyiko wa wanaume wote wa kundi hilo). Walijitenga katika miungano kulingana na sehemu zao za makaazi kando ya Bonde la Kerio na kando na Milima ya Cherangani.


Dini ya kiutamaduni ya Wamarakwet ilijumuisha miungu mingi zikiwa na uwezo na mamalaka yakutofautiana. Mungu wao wa umuhimu alikuwa Assis (jua), wakati mwingine alijulikana kama Chebetip chemataw . Alitambulika sana sana na baraka na heri njema. Mungu wao mwingine ni Ilat (mungu wa ngurumo za radi). Alitambulikana na mvua na wakati wa kiangazi sadaka zilitolewa ili kumpendeza. Alitambulikana pia na hasira na kisasi kwani alisababisha kiangazi na kuchapa watu na radi akiwa amekasirishwa.


Sehemu inayokaliwa na Wamarakwet ndiyo mojawapo wa sehemu za kupendeza sana na maumbile mazuri nchini Kenya, ikipakana kwa sehemu ya mashariki Mto Kerio ukiwa mita 1000 juu ya upeo wa bahari l, unaopitia katika sehemu ndogo ya Bonde la Ufa. Katika sehemu ya magharibi, inajumuisha sehemu yote ya milima ya Cherang’any ambazo urefu wake ni mita 3 300 juu ya upeo wa bahari magharibi mwa sehemu ya vilima ya Marakwet.


Makau makuu ya Wilaya ya Marakwet iko katika mji ulio kwenye mlima wa Kapsowar. Seheumu zingine za soko/miji ni Chebiemit, Kapcherop, Cheptongei, Arroor, Chesongoch, Chesoi, Kapyego, Tot, Sangach na Embobut Mosop.


Wamarakwet huongea lugha ya Kimarkweta. Ambayo inajumuisha Endow(Endoo), Kimala, Markweta na Sombirir na kadhalika.


Vita na majirani zao Wapokot[hariri | hariri chanzo]

Kabila za Wamarakwet na Wapokot zote ni kabila ndogo katika kabila kuu la Wakalenjin. Vita baina yao vilianza kwa sababu ya wizi wa Mifugo }, na kumekuwa na tangu hapo na nyakati za vita na amani. Vita vimekuwa vimekuwepo baina ya kabila za Wamarakwet kwa mfano, kapkau na karel kutoka bondeni kwa ajili ya mzozo wa shamba na umesababisha vifo vya watu (watu 11 waliuliwa kapkau). Kulikuwa na maandamano na wakaazi wa kata ya sambirir kwa madai ya mauaji ya watu na kuiomba serikali kufanya oparesheni ya ketika sehemu za chini ili kuondoa bunduki zote lakini hakuna kilichofanyika.Mkuu wa Wilaya aliwahakikishia kuwa atafanya awezavyo ili kufanya Marakwet mahala pa amani.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Marakwet of Kenya by Dr. Benjamin Edgar Kipkorir / F.W. Welbourn published in 1973 by the East African Literature Bureau.


  • 'The Expansion of Marakwet Hill-Furrow Irrigation in the Kerio Valley of Kenya' by W. Östberg. In Widgren, M. and Sutton, J.E.G. (eds.): Islands of Intensive Agriculture in Eastern Africa. James Currey publishers, Oxford, 2004 : 19-48.


Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]