Kaunti ya Trans-Nzoia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ikionesha eneo la Kaunti ya Trans-Nzoia, Kenya

Kaunti ya Trans-Nzoia ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010.

Wakati wa sensa ya mwaka 2019 wakazi walikuwa 990,341 katika eneo la km2 2,495.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 397 kwa kilometa mraba[1].

Makao makuu yako Kitale.

Iko katikati ya Mto Nzoia na Mlima Elgon.

Kihistoria, eneo hili limekuwa likikaliwa na Wakalenjin. Baada ya uhuru, mashamba mengi yaliyoachwa na Wazungu yalinunuliwa na watu kutoka makabila mengine ya Kenya.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Kaunti ya Trans-Nzoia imegawanyika katika maeneo bunge yafuatayo[2]:

Eneo bunge Kata
Kwanza-Mbunge Ferdinand Wanyonyi Kapomboi, Kwanza, Keiyo, Bidii
Endebess-Mbunge Robert Pokose Chepchoina, Endebess, Matumbei
Saboti-Mbunge Caleb Amisi Kinyoro, Matisi, Tuwani, Saboti, Machewa
Kiminini-Bissau Kiminini, Waitaluk, Sirende, Hospital, Sikhendu, Nabiswa
Cherangany-Mbunge Patrick Barasa Simiyu Sinyerere, Makutano, Kaplamai, Motosiet, Cherangany/Suwerwa, Chepsiro/Kiptoror, Sitatunga

Idadi ya wakazi katika kaunti ndogo (2019) [3][hariri | hariri chanzo]

  • Trans Nzoia West 202,377
  • Trans Nzoia East 229,538
  • Kwanza 203,821
  • Endebess 111,782
  • Kiminini 242,823

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30. 
  2. http://countytrak.infotrakresearch.com/Trans-Nzoia-county/
  3. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-13. Iliwekwa mnamo 2021-05-30.