Ruiru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Ruiru
Nchi Kenya
Mkoa Kati
Wilaya Thika
Mji wa Ruiru

Ruiru[1] ni mji katika Wilaya ya Thika, ipatikanayo katika Mkoa wa Kati nchini Kenya.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Mji huu uko katika umbali wa takribani kilomita 3 kutoka katika Mpaka wa Nairobi. unachukua ukubwa wa 292 km2 na umezungukwa na mashamba ya Kahawa. Ruiru ni moja kati ya miji inayotambulika zaidi nchini Kenya, ambao unaweza kufikika kwa urahisi kupitia barabara au reli.

Idadi ya Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1999, Ruiru ilikuwa na watu takribani 100,000. Hata hivyo, mji huu umekuwa na ongezeko la idadi ya watu, kutokana na uhaba wa nyumba Mjini Nairobi. Idadi ya watu mjini humo ilikadiriwa kuwa 220,000[2] Mji huu umeng'ang'ana kuwatosheleza wakazi wake.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Moja ya Majengo ya Ruiru

Wengi wa Wakazi wa Ruiru ni wanabiashara wa asili ya Kikuyu. Mji huu pia una matawi ya benki mashughuli kama vile Benki ya Equity, Benki ya Family, Benki ya Cooperative na Benki ya Barclays Pia kuna viwanda mbalimbali katika mji huo.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Wilaya ya Thika Mkoa wa Kati Barabara kuu ya Thika-Nairobi

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ukuaji wa Maeneo, Metropolitan Nairobi www.earth.columbia.edu
  2. Ruiru, Kenya: [1].

Anwani ya kijiografia: 1°08′56″S 36°57′25″E / 1.14889°S 36.95694°E / -1.14889; 36.95694